2018-01-15 15:45:00

Papa Francisko ataongoza Masifu ya Jioni tarehe 25 Januari 2018!


Tarehe 25 Januari 2018 saa 11.30 za jioni masaa ya Ulaya katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo, mjini Roma, Baba Mtakatifu Francisko ataadhimisha masifu ya jioni katika Sikukuu ya Uongofu wa Mtakatifu Paulo mtume wa watu, ikiwa ni hitimisho la Juma la  kuombea Umoja wa Wakristo. JUma la maombo hayo inayotarajiwa kuanza tarehe 18-25 Januari 2018 ikiongozwa mwaka huu na Kauli mbiu “ Mkono wako wa kulia ee Mwenyezi Mungu watukuka kwa nguvu”…(Taz. Kut 15, 6).

Watashiriki maadhimisho hayo  wawakilishi viongzo wote wa Makanisa na jumuiya za Kanisa zilizomo mjini Roma, na kwa njia hiyo wote wanaalikwa kuudhuria, kwa namna ya pekee makleri na waamini wote katika  jimbo Kuu la Roma.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.