2018-01-15 16:16:00

Maaskofu wa Venezuela wameitaka serikali kuinua hali za maisha ya watu!


Wakati hitimisho la Mkutano  wa mwaka wa Baraza la Maaskofu wa Venezuela huko Caracas, Maaskofu wametoa wito wa nguvu na kutangaza ujumbe huo kwa umma wakiwa wanatoa ushauri, lakini pia kushutumu vikali sera za kisiasa za serikali ambayo imesababisha nchi kuingia katika kipeo kibaya cha uchumi  na kuifanya nchi izidi kuongezeka umaskini, ukosefu wa ajira, rushwa na ufisadi, kwa ujumla ukosefu wa mambo msingi ya maisha ya kila siku, zaidi ukosefu wa matumaini endelevu kwa raia wake.

Ujumbe wa Baraza la maaskofu nchini Venezuela,unabainisha jinsi gani wazalendo wamekata tamaa kutokana na serikali kutojali watu wake au kuwatetea. Sababu hizo zimezua hasira kwa watu dhidi ya serikali ikionesha bayana mamilioni ya wanavenezuela kujaribu kukimbia nchi yao na kuelekea katika upeo mwingine kutafuta maisha bora. Na mzizi wa matatizo, ni kutokana na mipango ya sera za kisiasa na uongozi wa udikteteta. Ujumbe unasema, badala ya kuandika Katiba mpya, viongozi, wanatumia utawala wa kimabavu na uendeshaji kiholela wa mahakama kuu ya nchi kwa kuwakandamiza watu wengi. Aidha  serikali inazuia kila aina ya maandamano ya raia kutetea haki na sauti zao. 

Maaskofu wanabainisha kuwa, kwa sasa serikali imeendesha utawala wake, na kutawala raia ambao ni wa watu, lakini ambapo hakuna suluhisho lolote la matatizo ya raia wa nchi hadi kufikia kishinda kujikimu maisha yao ya kawaida.  Iwapo Serikali inazuia  kila aina ya uwezekano wa jamii ya umma kuwa mstari wa mbele wa maisha ya siasa, wanasema, ina maana ya ukosefu wa hali halisi ya uhuru na kusababisha matendo ya mivutano na ghasia dhidi ya serikali.
Viongozi wa serikali wanasahau kuwa watu wanao waongoza ndiyo wenye kauli ya mwisho; hivyo maaskofu wa Venezuela wanaomba serikali kuhakikisha pia uwazi hasa  baraza la ushauri wananapokaribia   katika mchakato wa uchaguzi wa rais mwaka huu .
Ujumbe wa maaskofu unatoa  ushauri kwa nguvu zote kwamba raia wasikate tamaa wakikumbuka  kauli mbiu ya Ziara ya Mtakatifu Yohane Paulo II nchini Venezuela 1996, iliyokuwa ikisema: ”amkeni na kujikita mbele maana ni wakati !

Wanabainisha kuwa, kuamka na kujikita maana yake ni kuwakumbusha viongozi walio  madarakani watende wajibu wao kwa mujibu wa watu wanao waongoza, wapinge kila aina ya utawala wa mabavu kwa sababu ya wema wa watu na taifa lao kwa ujumla. Nchi ya Venezuela inahitaji mabadiliko kamili.Serikali imeshindwa kazi yake ya kuhakikisha ustawi wa watu wake na jamii kama vile: huduma za umma, viwanda vya petroli, ukosefu wa ulinzi na usalama wa utakatifu wa umma,hata mashirika mingine  hawakuweza kutambua kujibu mahitaji ya watu. 

Kuhusiana na mchakato wa kupiga kura maaskofu wanasema kwa nyakati hizi ni zama za kidemokrasi ili kuweza kufikia mamadiliko ya kweli ya upeo wa nchi, hivyo Maaskofu wanaomba serikali kutoa hata ratiba kwa umma ya uchaguzi. Katika hilo pia wanataja maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyotamka hivi karibuni kwa wanadiplomasia,akitazama juu ya nchi ya Venezuela kwamb, ”Vatican ikiwa inajitahidi kujibu bila kusima mahitaji msingi ya watu, inawawataka serikali waweze kujita katika kuunda chomo madhubiti cha usimamizi  ili uchaguzi unaotarajiwa kufanyika uweze kupata suluhisho la migogoro iliyopo,na inaweza kutazama utulivu wa maisha endelevu ya watu wake.”

Maaskofu anasisitiza kuwa, uhuru ni haki ya binadamu isiyo pingwa na isiyo ya kununuliwa na pia dharura ya demokrasia. Kwa njia hiyo wanaonesha mshikamano wao na mamia ya wadau wenye mapenzi mema ya kisiasa, wafungwa  wa kila sababu, wagonjwa , wanafamilia na ambao wanaokosa kila aina ya haki zao msingi wakati wa michakato. Na ili wote  waweze kuwa na uhuru. Mashirika husika ya serikali wanapaswa kufuatilia michakato hiyo ya mashtaka, hasa unyanyaswaji wa watu na kutoa  kutoa adhabu kwa wahusika wanao kwenda kinyume na sheria.

Hata hivyo bado wanasema, mazungumzo na ushauri kati ya serikali na wawakilishi wa upinzani, ndiyo msingi mkuu na muhimu . Lakini pamoja na hayo lazima  kuhakikisha hali zote za watu zinakua nzuri na  utambuzi na kuheshimu katiba ya kweli ya kuongoza nchi. Kwa njia hiyo inaweza kuleta uaminifu na sifa kwa watu wanaotegewa.

Na mwisho maaskofu wanakimbilia ulizni wa Mama Maria , aweze kuwasindikiza watu hawa katika mateso mengi ya wananchi wa Venezuela. Na kwamna yeye ni mama wa hija ya hisotria ya wana wa Venezuela.
Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.