2018-01-15 15:56:00

18 Januari 2018, Mkutano katika Chuo cha Santa Croce kuhusu Msamaha!


Tarehe 18 Januari 2018 katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Santa Croce mjini Roma, utafanyika Mkutano kuhusu mada ya  msamaha. Mada hii ni msingi kutokana na kwamba, mara nyingi tabia ya kujisikia au kuwa na ukiburi inaweza kuchukua siku nyingi, hata kudumu kwa miaka. Msamaha ni kama jibu la suala hili, ambao unaweza kuponyesha majeraha ya mpasuko wa kina katika uhusiano kati ya mantiki  binafsi, ya familia, katika jumuiya na hata taifa. 

Kutokana na dhana hiyo, Chuo Kikuu cha Kipapa cha Santa Croce, kimeandaa mada ya kwanza  kuhusu suala hili la msamaha, mada itakayo waona washiriki wengi, hasa kuwaunganisha wataalam wa masuala ya mada hiyo kutoka nchi mbalimbali. Katika mada hiyo nyeti ya msamaha, wataalamu wataweza kujikita kwa kina kuzungumza na kueleza jinsi msamaha unavyoeleweka katika dunia ya Wakristo,wayahudi na waislam, hata njia gazi za kuweza kujikita katika matendo ya dhati, mathalani katika migogoro ya kisiasa. Watu wote wanaalikwa kudhuria.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.