Katika kipindi cha mwisho cha tafakari ya “Baba yetu” Kipindi ambacho kimeongozwa na Padre Marco Pozza, ambaye ni Padre Mhudumu wa gereza la wafungwa huko Padua, kwa kawaida mfululizo wa vipindi vyote 8 vimekuwa na wageni waalikwa,ambao ni ulimwengu wa walei waliobobea kwenye masuala ya utamaduni wa taifa pamoja na usanii mbalimbali, ambao walikuwa wakizungmza mara baada ya utangulizi wa Baba Mtakatifu kwa sala hiyo ya Baba Yetu.
Kwa njia hiyo Jumatano usiku wa tarehe 20 Desemba 2017 kilikuwa ni kipindi cha
9 katika mfululizo wa Sala ya Baba Yetu. Kipindi hiki kilianzishwa kwa ushirikiano
wa Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican na Kituo cha luninga Tv2000 kinachomilikiwa
na kuendeshwa na Baraza la maaskofu nchini Italia.
Katika vipindi hivyo “Padre nostro”, katika kuenzi sala ya Baba yetu na maisha ya
sala kwa mkristo, Kipindi kilikuwa na sehemu tisa, ambacho kimerushwa kila Jumatano,
majira ya saa 3 na dk 5 kwa saa za Ulaya.
Baba Mtakatifu akichambua Baba yetu na Padre Marco Pozza kwa kipinchi cha tisa
na cha mwisho amendelea kusema kuwa , tunasema kuwa sisi ni wakristo na tunasema kuwa
tunaye baba, lakini tunaishi, kana kwamba, ndiyo hasemi kama wanyama, lakini kama
vile watu ambao hawaamini katika Mungu na katika binadamu, wanaishi bila imani na
kuishi tukitenda mabaya, hatuishi kwa upendo bali kwa chuki, katika mashindano na
katika vita.
Baba Mtakatifu anauliza maswali, je Mungu anatukuzwa kati ya watu wanao pambana kati
yao kwa ajili ya mali? Je anatukuzwa katika maisha ya wale ambao wanafanya mipango
ya kiahalifu, ili kuweza kumwondoa adui? Je anatukuzwa katika maisha ya wale ambao
hawawatunzi vema watoto wao? Hapana, Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa, Mungu hawezi
kutukuzwa jina lake kwa namna hiyo!
Mafundisho ya Maneno ya Yesu yanatoa mwangwi katika matukio na maisha ya Baba Mtakatifu
Francisko katika wito wake wa kitume, na hasa kujikita katika mahangaiko na matumaini
ya wanawake na waamini wa sasa , hadi kuweza kugeuka kuwa na maisha yenye utajiri
wa maana na lengo.
Na kwa maana hiyo, Baba Mtakatifu anabanisha kuwa inahitaji ujasiri wa kusalia sala
ya Baba yetu. Inahitaji ujasiri wa kujiweka tayari kutamka “Baba” na kuamini kweli
kwamba Mungu ni Baba yetu ambaye ananisindikiza, ananihurumia , ananipatia mkate na
kuwa makini kwa kile ambacho mimi ninaomba na ananivalisha vizuri zaidi ya maua ya
kondeni . Kuamini hata hivyo ni ni tendo la kujiweka katika hatari na wasiwasi, kwa
maana unajiuliza maswali mengi kwamba, je ni kweli ninacho kiamini? . Lakini Baba
Mtakatifu anathibitisha kuwa ni vema kujaribu kuamini. Na ndiyo maana ni vizuri kabisa
kusali kwa pamoja, kwa maana tunasaidiana mmoja baada ya mwingine.
Baba Mtakatifu Francisko pia ametoa mfano wake binafsi kwamba,zamani walipokuwa watoto wadogo , walifundishwa kuwa mkate ulikuwa wa dhììthamani kubwa na ulipokuwa unaanguka, ilikuwa lazima kuookota , kuubusu na kuula. Kwa maana hiyo, mkate ni ishara ya umoja wa binadamu na ni ishara ya upendo wa Mungu kwa ajili yako anayekupatia mkate huo. Akiendeleza kufafanua juu ya historia hiyo binafsi, amesema, mikate iliyokuwa inabaki wakati wa kumaliza kula, bibi na mama walikuwa wakifanya nini? Waliifadhi vema na baadaye walichanganya na maziwa na kutengeneza keki au kitu kingine, lakini kamwe mkate haukutupwa.
Halikadhalika amesimulia tukio jingine kuwa, siku moja huko Buonos Aires ilifika Sanamu ya Mama yetu wa Fatima ikiwa inazungushwa na ambapo waliandaa misa ya wagonjwa katika uwanja mkubwa wa mpira ambao ulikuwa umejaa sana. Wakati huo Askofu alikwenda kuungamisha, na aliungamisha kabla ya Misa na baada ya Misa. Baba Mtakatifu anasema, mwisho hapakuwapo na watu maana walikuwa wote wametawanyika na kurudi makwao, wakati anakaribia kuamka, ili aondoke kwa maana alikuwa anasubiriwa sehemu nyingine ili kuweza kutoa kipaimara,alifika mwanamke mmoja mdogo. Huyo mwanamke alikuwa rahisi pia alikuwa amevaa nguo nyeusi utafikiri ni wanawake wakulima wa Kusini mwa Italia, ambao huvaa nguo nyeusi kipindi chote cha maombolezo.
Mwanamke huyo alikuwa na macho mang’avu yaliyokuwa yakimulika uso wake, na ndipo Baba Mtakatifu aliuliza swali kama alikuwa anataka kuungama, lakini akamwambia, “wewe hauna dhambi”. Mwanamke akamjibu kwa lugha ya kireno, “sisi sote tuna dhambi”. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu akasema, “kuwa makini: labda Mungu hasamehi” Mwanamke akajibu, “Mungu anasamehe kila kitu”…alijibu hayo kwa uhakika. Baba Mtakatifu akauliza “Je wewe unajaje?” mwanamke akajibu “ Kama Mungu hasamehi yote, dunia isingekuwapo”. Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema kuwa wakati huo alitaka kumwambia hivi wewe umesoma Chuo Kikuu cha Gregoriana!. Kwa mwaana hiyo Baba Mtakatifu amemalizia kwa kuthibitisha kuwa hiyo ni hekima ya watu rahisi,wanaotambua kuwa Baba yetu daima anawasubiri.
Ikumbukwe, katika makutano, maneno na majibu ya Baba Mtakatifu na Padre Marco Pozza, kimetolewa pia kitabu cha Baba yetu "Papa Francisko", kinachopatikana kwa sasa katika maduka ya vitabu mjini Vatican.
Sr Angela Rwezaula
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©. |