2017-12-20 08:59:00

Papa:Hata jangwani maua yatachanua,maana ni Bwana anatoa matunda!


Bwana mwenye kutoa matunda na anataka kila mmoja atoe matunda na kushi na wengine kwa kutoa maisha. Ni maneno taliyomo katika mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko siku ya Jumanne 19 Desemba kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican; akiwaalika watu watazame ndani ya holi la  mtoto Yesu wazi wakati wana msubiri pia kutazama ndani ya mioyo yetu ili isibaki imefungiwa kama kitu katika kutika jumba la maonyesho.

Utasa , ugumba  na kuzaa ni maneno mawili ambayo yamejikita sana katika mahubiri ya Baba Mtakatifu. Somo la kwanza linaeneelezea historia ya kuzaliwa kwa Samsoni na somo la pili kuelezea historia ya kuzaliwa kwa Yohane Mbatizaji ambayo ni habari njema inayoletwa na Malaika anaye walezea wanawake, mmoja tasa na mwingine miaka imepita ambaye ni Elizabet. Katika enzi zile, tendo la kuwa na tasa au mgumba, lilikuwa la aibu sana, lakini neema na zawadi kutoka kwa Mungu anakazaliwa mtoto. 

Katika Biblia , Baba Mtakatifu amesisitza kuwa inaonesha wanawake wengi ambao ni tasa na wanatamani sana kuwa na watoto au wengine wanalilia watoto, kwa ajili ya kuwapoteza, kwa mfano wa Sara, Noemi , Anna na Elizabeth. "Zaeni na mkaongezeke duniani", ilikuwa ni amri ya Mungu aliyo wapatia mababa zetu. Kwanjia hiyo,mahali ambapo yupo Mungu kuna matunda. Na kuzaa matunda mema katika Bublia ni Baraka. Hata hivyo Baba Mtakatifu ametafakari juu ya baadhi ya nchi ambazo wamechagua njia ya utasa,  pia  wanasumbuka sana na ugonjwa huo mbaya wa upungufu wa watoto katika nchi. Ameongeza kusema kuwa tunawatambua , kwa maana hawana watoto. Lakini siyo mali, bali nchi ambazo hazina watoto hazina baraka. Ndiyo ni kipindi cha mpito, kwa maana uzao daima umekuwa ni baraka za Mungu.

Kuna hata matunda mema ya kiroho yaani ya kutoa maisha. Mtu anaweza hasioe au kuolewa kama vile mapadre na walioweka wakfu. Lakini wanaishi maisha yao kwa kujitoa sadaka kwa wengine. ”Ole wetu sisi, Baba Mtakatifu anasisitiza, ”iwapo hatutui matunda kwa njia ya matendo mema”.
Kuzaa matunda ni ishara ya Mungu. Baba Mtakatifu katika hilo anakumbuka Nabii anaye chagua ishara nzuri ya jangwa.Ni kitu gani kipo zaidi katika utasa wa jangwa, wakati huo huo, nabii anasema kuwa, hata jangwani maua yatachanua,katika ukame yatatokea maji . Hiyo ndiyo ahadi ya Mungu ya kutoa matunda mema.

Ni kweli kwamba shetani anataka utasa, anataka kila mmoja wetu asiishi kwa ajili ya maisha yawe kimwili au kiroho na hata kwa kwa ajili ya wengine. Anayeishi maisha yake binafsi ni ubinafsi,ukiburi na ubatili na kunenepesha roho bila kuishi kwa ajili ya wengine. Ndiyo kazi ya shetani ambaye anafanya magugu mabaya yaote katika ubinafsi na kutofanya uzae matunda mema!

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.