2017-12-20 09:09:00

Papa amefanya mazungumzo kwa njia ya video na wanachuo kikuu cha Sofia Tokyo!


Baba Mtakatifu amefanya mazunguzo na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sofia cha Tokyo kwa njia ya video,mahali ambapo amewaelezea juu ya utashi wake wa kwenda  nchi ya Japan.Ni maangezi aliyo fanya asubuhi ya tarehe 18 Desemba 2017 kwa njia ya Video akiwa mjini Vatican na wanafunzi wa chuo Kikuu cha Sofia Tokyo nchini Japan. Ni maswali mengi yaliyomjia  Baba  Mtakatifu kutoka kwa wanafunzi hao, lakini kati ya maswali hayo wakacahgua ajibu maswali 8 tu.

Swali la kwanza lilikuwa ni kuhusu furaha kubwa zaidi aliyo wahi kupata; Furaha kubwa ya Baba Mtakatifu ni kukaa na watu na hivyo vijana wameuliza ni furaha  kubwa gani aliipata mara baada ya kuchaguliwa kuwa Papa. Akijibu amesema furaha siyo mara moja tu, bali mara nyingi amekuwa na furaha, hasa anapozungumza na watu, kwa namna ya pekee watoto, wazee na wagonjwa. Inamsaidia kukaa vizuri na wat, kwa njia hiyo pia inamfanya naye awe kijana na mwenye furaha kwa maana  ndiyo zaidi ya furaha.

Akijibu swali la pili kuhusiana na elimu ambayo anasema inalenga kujenga jamii ya mashindano, Papa amesema kuwa,wakati mwingi ipo hatari ya kuwa na mtazamo wa kuanagaliza nafasi ya kazi tu: Lakini elimu ni msingi kwanza kwasababu inakufanya ukue na kulimika kuwa mdogo, kwa maana ya kujishusha katika utoaji wa huduma yenye manufaa. Manufaa ni muhimu hasa unapotazama kuwa kitovu cha manufaa hayo ni kwa ajili ya jamii ambayo inastahili, ili kuweza kufanikiwa kwa maana kuna wakati mwingine inafikia hatua ya kuwa mbaya. Elimu isiyotazama huduma ya wengine Baba Mtakatifu anabainisha kuwa  ni elimu ambayo itaharibika. Elimu isiyopendeza na ambayo inajitazama yenyewe binafsi ni hatari ! Na kaulimbiu ya chuo Kikuu ni Elimu kwa ajili ya wengine, Chuo kwa ajili ya wengine kwa maana ya Chu cha huduma. Na ndiyo utajiri mkubwa huo, Baba Mtakatifu amesisitiza.

Swali jingine, Je ni waswasi gani mkubwa na matumaini ya Baba Mtakatifu kwa vijana wa leo hii? Na  Katika swali hili la tatu Baba Mtakatifu amejibu kuwa, wasiwasi wake ni ule wa kupoteza mzizi na kumbukumbu. Kwa maaa mizizi ya utamaduni, mizizi ya historia, mizizi ya familia  na mzizi ya binadamu.
Na Vijana kukua bila mzizi hawawezi kupata uwezo wa kuendelea na kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anaongeza kusema kuwa, njia sahihi ya kuweza kupata mizizi ni kuwatia moyo vijana na ili wapate  kuzungumza na wazee. Je kijana anapaswa kufanya nini? Lazima afanye kumbukumbu, yaani kutafuta mizizi ambayo si kuitunza katika kabati, bali kuzungumza , kujadiliana na wakati wa sasa, kwa kutazama upeo endelevu. Mizizi hiyo mbele ya changamoto za wakati  wa sasa itaweza kutoa matunda ya kesho na kuchanua. Vijana hawawezi kusimamishwa, bali wanapaswa kuwa katika mwendo daima na  kutembea kuelekea ahadi, lakini yenye kujikita katika mzizi yao daima  na kukabiliana changamoto za wakati uliopo. Amesisitiza zaidi kwamba,ni kwa njia ya vijana dunia inabadilika moja kwa moja!

Katika swali la nne lilikuwa linahusu juu ya dini ambayo inafanya ukue na kuwa binadamu, ambapo Baba Mtakatifu amejibu kwa kusema, dini siyo tamthilia ya kutungwa, bali inazaliwa na shahuku ndani ya moyo wa binadamu tangu hawali kutoka kwa aliye juu na ambayo katika ukuaji wake kutoka kwa aliye juu  inapata msingi ulio mkuu ambao ni Mungu. Na Kila dini Baba Mtakatifu amebainisha kuwa, inakufanya ukue. Lakini iwapo  unaweza kukutana na mtu ambaye anakueleza kuwa ni mtu wa dini wakati huo huo  hakui, wala hatoi huduma kwa wengine, basi huyo siyo mtu wa dini bali anaabudu miungu.
Mtu huyo anatafuta manufaa binafsi kwa kutumia dini. Kila aina ya ukubwa wa dhati wa dini, unafanya kukua na zaidi wakati ikiwa inakufundisha kutazamia yaliyo juu zaidi yake, inakufundisha pia kuwa na uhusiano na wengine. Dini inakufanya ukue na watu wakubwa wa historia ya binadamu, hao walikuwa na watu wa dini, amesisitiza Papa.

Hata hivyo ameendelea kusema , maonesho ya kikristo ambayo yeye binafsi anaamini na hata wakristo wengie, ni kama kwamba ni kanuni msingi wa kuabudi Mungu na kutoa huduma kwa wengine. Iwapo mkristo hana tabia ya kuabudu  Mungu na kutoa huduma  kwa wengine, huyo si mkristo. Kwa maana atajisemea kuwa ni mkristo lakini ki ukweli si mkristo: Kwa kufafanua zaidi juu ya suala hilo, Baba Mtakatifu amesema juu  ya matukio ya itikadi za kidini kwamba,  kila imani ya dini, inayo makundi madogo ya wafuasi wake wa kiitikadi ambao wakati mwingine wanakwenda kinyume na mawazo ya dini hadi  kusababisha matukio ya  kigaidi.

Swali la tano lilikuwa linahusu kuhusu mazingira na umaskini, hivyoBaba Mtakatifu amejibu kuwa, binadamu wa leo anajikuta mbeleya uchaguzi wa lazima. Au kuchukua hatua ya kufikiria mazingira au kwenda katika mwelekeo wa vizingiti vya uharibifu wa binadamu. Katika suala hili, amewapa mfano wa kukutana mjini Vatican na baadhi ya viongozi wa nchi zinasoishi katika  Mabahari Makuu, ambao aliweza kuwaeleza juu ya tishio la baadhi ya visiwa ambayo vinakaribia kupotea kati ya miaka 20, ijayo kutokana na kwamba bahari imeongezeka ujazo wake, kwasababu ya ongezeko la joto duniani. Na kwa njia hiyo ni zipo nchi ambazo kwa miaka michache zipo hatari ya kupotea.

Ameongeza kuwaeleza kuwa, ni lazima kuwajibika na kuwa na ulinzi wa ardhi yetu wote. Pamoja na hayo ameelezea juu ya ukataji hovyo wa misitu kama vile Amazon au katika misitu mikubwa ambayo ameeleza ni hewa ya  Oksijeni ya binadamu: ukataji hivyo wa misitu unasababisha uyumbaji mkubwa wa dunia. Na kwa namna hiyo amewaonya  wale wote wenye kujihusha na uchumi ambao amesema, wanatazama maslahi yao binafsi. Na kwa njia hiyo hiyo anasema haiwezekani kabisa  kuhudumia fedha tu, utafikiri ndiyo jambo pekee linalohitajika katika maisha ya binadamu. Ukosefu wa msimamo wa ekolojia unasabaisha ukosefu wa usawa kijamii,na ambao unatengeneza umaskini mpya katika dunia hii. Na umaskini huo Baba Mtakatifu amebainisha kuwa unaongeza kwasababu ya kuweka fedha kwa ndiyo kitovu cha mfumo mzimwa wa uchumi duniani.

Akijibu swali la sita ambalo mwanafunzi ameuliza juu ya tabia ya Papa na ili aweze kujifafanua mwenyewe kwa maana watu wengi wanaongea sana juu yake na sifa nyingi, lakini Baba Mtakatifu amesema kuwa tunapokuwa tunachana nywele, tunanawa usoni, tunajitazama kwenye kioo. Na iwapo kioo kinakuwa sehemu yako ya maisha, mara nyingi  unaanza kujiuliza katika kioo kwa tabia ambayo wakati mwingiine amesema hujitambui wewe mwenyewe!
Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu amesema, jambo zuri anafikiri ni muhimu kuwa makini na kutafuta kujihukumu binafsi. Lazima kuwa makini usije kuangukia kwa kujitathimini katika kioo. Kwasabau kioo kinadanganya na kitadanganya daima. Kwa njia hiyo, akijibu swali hilo kuhusu yeye binafsi ni nani, amesema kuw, anatafuta kutojiangalia  katika kioo ambacho kinalazimisha l kila wakati kujitazama,na  wakati huo huo ubatili inaweza ukakusumbua kila uendeko.

 Kwa njia hiyo badala ya kujitazama katika kioo, yeye anatafuta mara mbili au mara nyingi kutazama ndani ya mambo ambayo amesikia wanasema kwa siku, mambo ambayo yamemtukia kwa siku , ili kuweza kujihukumu menyewe kile ambacho amefanya au ametoa uamuzi au kazimia jinsi atakavyokuwa na hivyo anafikiria kuwa yeye ni mdhambi ambaye Mungu amempenda sana na anampenda bado. Na hivyo hilo linamfanya awe na furaha
Swali la saba lilikuwa linahusu juu ya wakimbizi ambao Papa amejibu kuwa leo hii ni matatizo makubwa hasa yanayohusu historia ya binadamu. Binadamu ni muhamiaji. Ulaya leo hii imejengwa na wahamiaji ambao waliofika kwa mihongom mingi kutoka katika mabara mengine. Watu wa Ulaya siyo asili ya kuzaliwa bali ni wa Ulaya. Wana asili ya uhamiaji. Tatizo la uhamiaji Ulaya, Baba Mtakatifu anasisitiza, ni janga kubwa baada ya Vita ya Pili ya Dunia na ni tatizo ambalo tunapaswa kukabiliana nalo.

Mhamiaji anayekimbia vita na njaa, si rahisi kumkataa. Ni mtu anayetakiwa apokelewa na kushirikishwa. Hiyo ina maana ya kutofungia katika mipaka na . Kushirikisha ni kupokea mtu na kumpa mafunzo au kazi. Kinyume na hayo, kumbagua na kumwacha mtu upweke, unaweza kusababisha matatizo dhidi ya amani na katika kuundwa kwa makundi ya kigaidi. Mchakato wa kucanganyikana na familia mpya  ni muhimu kwa maana pia wanazaliwa wengine na  kutokea ushirikishwaji mwema wa watu wote.

Sr Amgela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.