2017-12-15 16:54:00

Salam za Papa kwa Wasanii wa Tamasha la Noeli Vatican 2017!


Baba Mtakatifu amekutana na kuzungumza na wasanii wa Tamasha la Krismasi mjini Vatican, tarehe 15 Desemba 2017, mahali ambapo amewapongeza kwa ushiriki huo wa Tamasha la nyimbo za “Noeli Vatican”. Baba Mtakatifu amesema kuwa  Mchango utakao patika katika tamasha hili utawezesha kuendesha mipango kwa ajili ya watoto wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kwa ajili ya vijana wa Argentina. Aidha amewasalimia wote walio andaa tukio hili, hata ambao wataendelea na  tamasha hilo Jumamosi usiku tarehe 16 Desemba 2017; pia watakao shiriki kwa namna moja au nyingine katika kujitoa na kuenzi mahitaji ya wenye shida, ambao wanaomba msaada na mshikamano.

“Noeli ni sikukuu inayosikika,inayoshirikisha,yenye uwezo wa kuwasha mioyo yenye baridi, na kuondoa vizingiti vya utofauti dhidi ya jirani, inatia moyo wa kujifungua kwa ajili ya mwingine na kujitoa bure bila kubakiza”. Na kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anaongeza, “kuna haja leo hii ya kuhamasisha ujumbe wa amani na undugu katika sikukuu hii ya kuzaliwa kwa Bwana; kuna haja ya kuwakilisha tukio hili ili kuelezea hisia za kweli zinazoihusu”.

Halikadhalika ameeleza, “kazi ya usanii ni chombo muhimu katikati, kwa ajili ya kufungua milango ya akili na moyo kuelekea maana ya kweli ya Noeli. Ubunifu na akili ya wasanii, na kazi zo, hata kwa muziki na nyimbo vina uwezo wa kufikia wadau na watendaji kwa kina katika dhamiri. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anawatia moyo ili Tamsha la Noeli Vatican, liweze kuwa fursa ya kupanda huruma, amani na mapokezi yatokanayo katika Holi la Betlehemu. Na kwa kila mmoja wao anampogeza na kuwatakia,utulivu wa Sikukuu zote za kuzaliwa kwa Bwana zenye kuwa na utajiri wa furaha na amani. Mwisho Amewabariki!

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.