2017-12-15 17:05:00

Papa amekutana na Rais Juan Evo Morales Ayma wa nchi ya Bolivia


Tarehe 15 Desemba 2017, Baba Mtakatifu Francisko asubuhi amekutana na kuzungumza na Rais wa nchi ya Bolivia mjini Vatican, Bwana Juan Evo Morales Ayma. Mara baada ya mkutano huo amekutana na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, akisindikizana na Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher. 

Katika mazungumzo yao wameonesha furaha kuhusu uhusiano mwema na  mshikamano kati ya Vatican na nchi hiyo hasa kwa mchang ambao Kanisa linachangia ili kuhakikisha maendeleo ya binadamu, jamii na utamaduni wa watu wa nchi hiyo, pia uhusiano katika Vatican na Bolivia na mada nyingine za sasa zinzohusu  pande zote mbili za nchi.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.