2017-12-13 14:46:00

Papa:Misa Takatifu Vatican kwa ajili ya Heshima ya Mama Maria wa Guadalupe


Tutazame utajiri na utofauti wa tamaduni za watu wa Amerika ya Kusini na wa Caribien na kuwatetea kwa ujasiri. Ni wito wa Baba MtakatifuFrancisko wakati wa mahubiri yake, kwa siku ya tarehe 12 Desema 2017, saa 12:00 jioni masaa ya Ulaya, wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kwa tukio la Sikukuu ya Mama Maria wa Guadalupe, msimamizi wa Bara la Amerika ya Kusini. Ni mwaka wa nne mfululizo, Baba Mtakatifu akiadhimisha sikukuu hiyo ya Msimamizi wa Amerika ya Kusini katika maadhimisho ya liturujia kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican.

Akitafakari Injili ya siku ambayo ilikuwa inaelezea ya sura ya Elizabeth, Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa, huyo ni mwanamke akiwa chini ya ishara ya utasa na chini ya ishara ya kuzaa, lakini anayefanana na sura ya Juan Diego, maskini muhindi mwekundu, ambaye Mama Maria alimtokea tarehe 9 Desemba 1531 katika kilima cha Tepeyac, kaskazini mwa Mji wa Mexco. Mama Maria, alimchagua kama mjumbe wake kwa ajili ya kujenga Kikanisa, katika eneo hilo, na mahali ambapo aliweza kushinda vizingiti vya mwanzo kutokana na askofu kutoamini maneno yake, hadi siku tatu baadaye, tarehe 12 Desemba ilipojitokeza sura ya Mama Maria katika kitambaa cha kanzu la kijana Juan Diego.

Baba Mtakatifu akiendelea na maelezo ya historia ya Diego anasema: kijana mwekundu, alihisi kutostahili mbele ya utume  aliyopewa na Maria, ndiyo kama ilivyokuwa kwake Elizabeth, kwa maana, kwa mujibu wa mila na desturi  za wakati ule, yeye alikuwa akiishi na utasa kama ishara ya aibu katika mwili wake.(“Esterilidad que puede tomar muchos nombres y formas…….”).

Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu amefafanua: utasa unaweza kuchukua majina mengi na aina nyingi, hasa kila mara mtu anapohisi katika mwili wake aibu, akitazama jinsi gani anavyo telekezwa au kusikia maneno mengine juu yake. Pamoja na hayo, hisia hizo zinawezekana hata leo hii kuwapo katika jumuiya ya watu wa asili, Waafro na watu kutoka Amerika ya Kusini ambao mara nyingi na  katika hali tofauti, hawatendewi haki, hasa zaidi kwa upande wa ukosefu wa  hadhi na usawa wa hali ya maisha, kama walivyosema Maaskofu wa kanda hizo, katika Waraka wao wa  mwisho wa Mkutano Mkuu wa  Baraza la Maaskofu wa Amerika ya Kusini.

Elizabeth aliyechukua mimba pamoja na uzee wake, anastaajabu, anaimba kwa mema yote aliyotendewa na  mara baada ya kutembelewa na Maria, anamtambua kuwa ni mama wa Bwana. Na ndiyo ilivyokuwa hata kwa kijana Juan Diego alipotokewa na Bikira Maria “Morenita”. Kutokana na matukio kama hayo, Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, inajieleza kuwa Mungu bado anaendelea kutuonesha kuwa,”jiwe walilokataa waashi limekuwa jiwe la pembeni”. Na kwa njia hiyo, anatoa ushauri wa kutambua na kusifu utofauti wa utamaduni (“…ella es signo de la gran riqueza…..”)

Kwa maana  anamesema, ni ishara ya ukubwa wa utajiri ambao tumealikwa kuhamasisha, hasa katika nyakati zetu, ili kuweza kutetea kwa ujasiri dhidi ya jaribio lolote ambalo linataka kufananisha na matokeo yake huishia itikadi zenye kuwa na lengo katika fikira, hisia ya maisha, ambayo huishia bila kutoa chochote na kubaki tasa, bila kutoa urithi wowote kutoka kwa babu zetu, na kuwafanya watu wahisi, hasa vijana wetu ukosefu wa kurithi chochote kwasababu wao wanatokana na kizazi hicho  au utamaduni mwingine.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.