2017-12-13 14:30:00

Papa:Kwenda Misa siku ya Jumapili ni kukutana na Bwana na kupumzika!


Ndugu wapendwa,tuanze tena kwa upya safari ya Katekesi kuhusu Misa, leo hii tujiulize lakini kwanini tunakwenda Misa siku ya Jumapili? Maadhimisho ya Ekaristi Siku ya Jumapili ni kiini cha maisha ya Kanisa (taz Katekisimu ya Kanisa Katoliki n.2177) Sisi kama  wakristo tunakwenda katika Misa ya Jumapili ili kukutana na Bwana Mfufuka  au kuacha ukutane na Yeye, kusikiliza Neno lake na kulishwa katika meza yake, kwa maana hiyo, kuwa Kanisa au kwa kuwa Mwili hai katika ulimwengu.

Ni utangulizi wa Maneno ya Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko, katika mwendelezo wa Mada ya Misa katika katekesi yake,tarehe 13 Desemba 2017 kwenye ukumbi wa Mwenyeheri Paulo VI mjini Vatican, akiongozwa na Injili ya Mtakatifu (Yh  20, 1. 19-23 ) mahali ambapo Mwinjili Yohane anasimulia siku ya Alfajiri mapema Jumapili kukiwa bado na giza Maria Magdalena aliwekwenda kaburini, akaliona jiwe limeondolewa mlangoni pa kaburi.

Baba Mtakatifu anasema, mitume wa Yesu waliyatambua tangu mwanzo kwa maana waliadhimisha makutano ya Ekaristi na Bwana kila siku katika juma, ambapo wahayahudi walikuwa wakiita “siku ya kwanza ya juma” na Waroma wakiita “ siku ya jua”, kwasababu ni siku hiyo, Yesu alipofufuka katika wafu na kuwatokea mitume, akazungumza nao, akala nao na kuwapatia Roho Mtakatifu (Taz Mt 28,1; Mk 16,9.14; Lk 24,1.13; Yh 20,1.19) kama ilivyosikika katika Biblia.

Hata matukio ya uvuvio wa Roho katika siku ya Pentekoste ilitokea siku ya Jumapili na ilikuwa siku ya 50 baada ya ufufuko wa Yesu. Na katika kanda zile, Jumapili ni siku takatifu kwetu , inajitakatifuza katika maadhimisho ya Ekaristi, uwepo hai wa Bwana kati yetu na kwa ajili yetu. Ni Misa inayofanya Jumapili kikristo! Jumapili ya kikristo inazunguka yenyewe katika misa. 

Je ni Jumapili ambayo kama mkristo anakosa kukutana na Bwana? Ndiyo, Baba Mtakatifu anauliza swali hilo na kujibu, kwa maana, kuna baadhi ya jumuiya za kikristo kwa bahati mbaya hawawezi kunufaika na Bwana kila Jumapili: lakini pamoja na hayo siku hiyo takatifu inawaalika wote  kujikita katika sala kwa jina la Bwana, kusikiliza Neno la Mungu na kuwa na matamanio  hai ya Ekaristi ndani ya mioyo yao. 
Katika thamani hizi, bado kuna mwalimu Ekaristi, yaani siku ya Jumapili baada ya Jumapili. 

Kwa maana hiyo Mtaguso wa Pili wa Vatican, ulitaka kusisitiza kuwa Jumapili : Jumapili ni siku ya sikukuu ya lazima ambayo inapaswa kupendekezwa na kufundishwa kwa waamini, hivyo pia inakuwa siku ya furaha bila ya kufanya  kazi.(Cost. Sacrosanctum Concilium, 106).
Katika jamii zilizogubikwa na malimwengu,zimepoteza maana hiyo ya ukristo siku ya Jumapili inayoangazwa na Ekaristi. Hiyo ni dhambi!  Baba Mtakatifu anaonesha masikitiko. Katika mantiki hizi ni lazima kuamsha kwa upya utambuzi na kufufua maana ya sikukuu, na si kupoteza maana ya sikukuu, kwa maana ya furaha, katika jumuiya za parokia, katika mshikamano na katika kupumzika na kulainisha roho na mwili.(Katekisimu ya Kanisa Katoliki nn.2177-2188).

Katika thamani hizi mwalimu ni Ekaristi ya Jumapili baada ya Jumapili:Tendo la mapumziko ya Jumapili bila kazi haikuwa tu katika karne za kwanza: kwa maana ni uhusiano maalumu wa Ukristo. Katika historia ya utamaduni wa kibiblia,Wayahudi walikuwa wanapumzika siku ya Jumamosi, wakati huo huo katika jamii ya waroma hapakuwapo na mtazamo ya mapunziko kutokana na watumwa kutumikia. Na ndiyo maana ikatokea maana ya ukristo yaani wa kuishi kama watoto na siyo watumwa, ambao wanaongozwa na Ekaristi na kuifanya siku ya Jumapili iwe ni siku ya mapumziko karibu duniani kote.

Bila Kristo tunahumiwa kutawaliwa na uchovu wa kila siku, wasiwasi wake,na hofu ya kesho. Kukutana na Bwana siku ya Jumapili, inatia nguvu za kuishi leo hii na imani na ujasiri na kwenda mbele na matumaini. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, sisi Wakristo tunakwenda kukutana na Bwana siku ya Jumapili katika maadhimisho ya Ekaristi Takatifu.

Muungano wa Ekaristi na Yesu , Mfufuka na anayeishi daima inajidhirisha katika Siku ya Jumapiliisiyo kuwa mawio ya jua, mahali ambapo hapatakuwapo na uchungu na maombelezo wala machozi, bali furaha ya kuishi kwa dhati na daima na Bwana. Kwa maana hiyo hata mapumziko ya heri yanazungumzwa na Misa ya Jumapili, kwa kufundisha kwa kupita juma baada ya nyingine tukijikabidhi mikononi mwa Baba yetu aliye mbinguni.

Baba Mtakatifu ametoa baadhi ya maswali ya kujiuliza: tunawezaje kuwajibuje wale ambao wanasema haisadii kitu kwenda katika misa na hata Jumapili, je ni umuhimu gani wa kuishi vema kwa kupenda jirani? Anajibu kwamba, ni dhahiri kuonesha kuwa, ubora wa maisha ya kikristo unapimwa kutokana na uwezo wa kupenda kama alivyosema Yesu kwamba: “ kwa maana hiyo watawatambua kuwa ninyi ni wafuasi wangu: mkipendana ninyi kwa ninyi  (Yh 13,35); Je tunawezaje kuweka katika matendo Injili bila kuchota nguvu muhimu ya kufanya hivyo, katika siku ya Jumapili na baaaye, ikiwa ndiyo kisima kisichoisha cha Ekaristi?

Kwa kujibu hayo maswali amesema; Kwena katika Misa si kwa ajili ya kumpa chochote Mungu bali ni kupokea kutoka kwake kile ambacho tunahitaji. Tunakumbushwa katika sala ya Kanisa kwa Mungu:Wewe huhitaji sifa yetu, lakini zawadi ya upendo wako unatuita kutupatia neema; nyimbo zetu za baraka haziongezei ukuu wako, bali zinatupatia neema inayotukomboa.

Kwa kumalizia, kwa nini kwenda Misa siku ya Jumapili? Haitoshi kujibu kwamba ni amri ya Kanisa; hii husaidia kuhifadhi thamani yake, lakini haitoshi peke yake. Sisi Wakristo tunahitaji kushiriki katika Misa ya Jumapili kwa sababu tu ni kwa neema ya Yesu, pamoja na uwepo wake wa kuishi ndani yetu na kati yetu, tunaweza kutekeleza amri yake, na hivyo kuwa mashahidi wake wa kuaminika.

Ujumbe wa Papa Francisko baada ya Katekesi kwa NGOs:Kufanya kazi kwa roho ya pamoja na mshikamano na Mashirika yasiyo ya kiserikali katoliki (NGOs)na wawakilishi wa Vatican, ambao ni ishara ya wajibu wa Kanisa katika ujenzi wa dunia yenye kuwa na haki na mshikamno. Ndiyo maneno yake BabaMtakatifu Francisko , mara baada ya Katekesi yake Jumatano 13 Desemba 2017 katika ukumbi wa Mwenye heri Paul Vi Vatican, aliyo walenga wawakilishi wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya kiserikali lakini ambayo ni yenye roho ya kikatoliki, ambao wameunganika katika jukwaa lao siku hizi mjini  Roma.

Baba Mtakatifu Francisko anawatia moyo Mashirika hayo yasiyo ya kiserikali, lakini ya roho Katoliki  kwa ajili ya kutetea na kulinda hadhi ya binadamu waendelee na jitihada hizo. Amependa kuwapongeza kwa ajili ya juhudi zao za kupeleka mbele Injili kwa mitindo mbalimbali katika maeneo tofauti na hasa ya pembezoni mwa dunia, ili kulinda na kutetea hadhi ya binadamu na kuhamasisha maendeleo kamili ya watu na ili kuweza kukabiliana na mahitaji ya kimwili na kiroho kwa watu wengi katika familia yetu ya binadamu.

 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.