2017-12-11 16:44:00

Vatican: Festa della Madonna di Guadalupe


Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 12 Desemba 2017 ataadhimisha kumbu kumbu ya Bikira Maria, Mama Yetu wa Guadalupe, ambapo ataungana na mamillioni ya familia ya Mungu kutoka Amerika ya Kusini kuadhimisha Ibada ya Misa takatifu kwa ajili ya heshima ya Bikira Maria Mama yetu wa Guadalupe. Ibada hii inatarajiwa kuanza saa 12:00 jioni kwa saa za Ulaya, lakini itatanguliwa kwa Ibada ya Rozari takatifu,  Waamini na wanadiplomasia kutoka katika nchi za Amerika ya Kusini wanaowakilisha nchi zao mjini Vatican wanatarajiwa kushiriki kwa wingi. Kwa mara ya kwanza kumbu kumbu hii iliadhimishwa mjini Vatican tarehe 12 Desemba 2011 na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI kama kumbu kumbu ya Jubilei ya uhuru kwa nchi nyingi za Amerika ya Kusini. Kunako mwaka 2014, Baba Mtakatifu Francisko akaonesha nia njema ya kutaka kuadhimisha Ibada ya Misa takatifu kwa ajili ya kumbu kumbu ya Bikira Maria wa Guadalupe. 

Pia Kwa bahati nzuri Baba Mtakatifu Francisko alibahatika kutembelea Mexico kuanzia tarehe 12- 18 Februari 2016 pamoja na kutoa heshima zake kwa Bikira Maria, Mama Yetu wa Guadalupe. Mama maria anayeheshimiwa sana katika Bara la Amerika ya Kusini na Marekani.


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.