2017-12-09 16:16:00

Papa:Mtakatifu Francesca Cabrini ni mmisionari wa nyakati za sasa!


Mtakatifu Francesca Cabrini  ni mmisionari wa sasa aliye makini katika mahitaji ya binadamu ya kila siku. Huo ndiyo mfano wa kweli wa wito hasa wa  kujisahau na kujiweka wakfu moja kwa moja  katika upendo wa Mungu. Ndiyo maneno yake na msisitizo mkubwa  katika kueleze  maana ya maisha ya Mtakatifu Franciska Cabrini, aliyozungumza Baba Mtakatifu Francisko  kwa  Wamisionari wa Moyo Mtakatifu wa Yesu aliokutana nao katika Ukumbi wa Clementina, mjini Vatican, tarehe 9 Desemba 2017.

Wamisionari hawa wanaadhimisha jubilei ya Miaka 100 tangu kifo cha Mkatifu mwanzilishi wa Shirika hilo na ambaye ni  mtakatifu msimamizi wa wahamiaji. Baba Mtakatifu anasema, huyo alikuwa ni mmisionari wa kweli aliye tambua  kuishi akitazama mbele kwa kuiga mfano wa Mtakatifu Francisko Xavier. Akifafanua juu ya wito wake anasema, yeye alikuwa anaota ndoto ya kuwa mmisionari mkubwa, ili afike katika nchi ya China, lakini wakati huo huo ulikuwa ni muda mfupi ameanzisha Shirika la Wamisionari wa Moyo Mtakatifu wa Yesu. Mungu alikuwa na ndoto nyingnie na ishara tofauti na mawazo hayo; kwa maana hiyo inajidhihirisha wazi kwani, ni Papa Leo XIII aliyebadilisha mawazo hayo, badala ya kwenda mashariki,  Cabrini alikwenda Magharibi.

Safari hiyo ndiyo alipoanza utume huo. Karama yake kwa nyakati za sasa ni muhimu na kuhitajika kwasababu inahusu wahamiaji, wenye kuhitaji, pamoja na  kutafuta sheria nzuri na mipango ya maendeleo, Baba Mtakatifu anaongeza kwamba, zaidi ya mipango hiyo,watu hao wanahiaji kusikilizwa, kutazamwa kwa macho yenye huruma na uelewa na kusindikizwa: wanahitaji Mungu, katika kukutana nao kwa upendo uliotolewa bure na Mungu, katika kukutana na mwanamke mwenye roho ya kujiweka wakfu kwa Mungu na jirani ambaye anakuwa kama dada na mama.

Halikadhalika akisistiza juu ya Mtakatifu Francesca Cabrini anaongeza kusema, alikuwa mama jasiri katika maisha yake na mwenye uwezo wa kazi, kwa kusafiri kwenda  mbali zaidi ya  bahari, ambapo akafanya kauli mbiu ya Mtakatifu Paulo isemayo“ Yote nayaweza kwa yule alinapaye nguvu”(Fil 4,13) kuwa yake kweli! Kwa kwa kuongozwa na muungano na Kristo, miaka michache aliweza kuanzisha matendo ya huruma 67. Matendo hayo ni mashule vyuo, mahosptali, nyumba za yatima na mahabara mbalimbali.

Kwa mujibu wa Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, kumfanya kumbukumbu ya kijana Mtakatifu huyo, ni wito wa nguvu  kwa sisi sote, tunaalikwa kutangaza, kwa njia ya kutambua na kupokea ishara za nyakati, kuzisoma na kuzitafakari katika mwanga wa Neno la Mungu ili kuweza  kuishi kwa namna ya kutoa majibu ya kina ambayo yanamfikia kila mtu, kama alivyo fanya Mtakatifu Franciska Cabrini.

 Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.