2017-12-07 16:12:00

Papa:Tuondokane na vikwazo juu ya Luteri na wakatoliki wasiwe kamwe maadui!


Baba Mtakatifu amekutana na wajumbe wa Shirikikisho la Kiluteri  duniani mjini Vatican  walioongozwa na Askofu Mkuu wa Nigeria Musa Panti Filibus  ambapo ametoa salam na pongezi kwa Dk. Junge, Katibu Mkuu na Mwenyekiti Msaidizi na wajumbe wa Shirikisho la Kiluteri Duniani, kwa hotuba na kumpongeza kuchaguliwa kwake hivi karibuni.

Hotuba hiyo akielekeza kwa Askofu Mkuu Musa anasema, kwa pamoja wanaweza kufanya kumbukumbu kama maandiko matakatifu yanavyofundisha  kuwa Mungu ametutendea makuu! (Zab 77,12-13). Baba Mtakatifu anasema, kumbukumbu ni kwa namna ya pekee katika vipindi vyote vya mikutano ya  kiekume vilivyofanyika katika kipindi chote cha mwaka wa maadhimisho ya kumbukumbu ya mageuzi ambayo imehitimisha siku chache zilizopita. Aidha anongeza kusema, anapenda kukumbuka hasa  tarehe 31 Oktoba 2016 waliposali pamoja huko Lund Sweden, mahali lilipoanzishwa Shirikisho la Kiluteri duniani. 

Ilikuwa ni jambo muhimu kukutana, hasa katika salam na ili si katika mipango ya kibinadamu, bali kwa neema ya Mungu, vichipukizi viweze kutoa zawadi ya umoja kati ya waamini. Na hivyo ni kwa njia ya sala tu, inawezekana kulinda mmoja na mwingine. Sala inatakasa,inatoa nguvu,inaangaza njia na kufanya kwenda mbele. Sala ni kama petroli ya katika safari ili kuelekea umoja wa kweli. 

Hiyo inajidhihirisha katika upendo wa Bwana utokanao na kusali, umoja unajikita katika nguvu ya upendo ambao unatufanya kukaribiana, kuwa na uvumilivu kutokana na mabadiliko ya uongofu na nguvu ya kwenda mbele pamoja. Ni kuazia katika sala ndipo inawezekana kuwa na roho ya mabadiliko ya kiekune na vishirio vya umoja, pia mazungumzo yanajengwa na kuonekana katika msingi wake.

Aidha akitafakari juu ya sala anasema, ni kutazama juu ya historia iliyopita na kumshukuru Mungu , kwasababu mgawanyiko japokuwa ulileta uchungu ambao ulisababisha kuwa mbali kwa mihongo mingi, kwa bahati katika miaka ya mwisho imeonesha hatua myeti ya safari ya kuelekea katika umoja ambayo ni safari ya kiekuemene, inayotokana na nguvu ya  Roho Mtakaitfu. Njia hiyo imetufanya kuchilia mbali vizingiti vilivyojitokeza kipindi cha Martin Luteri na juu ya hali haisi  ya Kanisa Katoliki katika kipindi hicho.

Safari ya kiekumene imechangia kwa kiasi kikubwa mazungumzo  katika Shirikisho la Kiluteri Duniani na Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuhamasisha umoja  wa Wakristo,ulioanzishwa tangu mwaka 1967. Mazungumzo ambayo yanafanya kumbukumbu ya shukrani leo hii  kwa miaka 50 iliyopita; ni kutambua baadhi ya maandiko muhimu ambayo ni Mkataba wa pamoja juu ya Mafundisho ya haki na Waraka kutoka kipindi cha migogoro kufikia umoja.

Katika kumbukumbu ya utakaso leo hii, tunaweza kutazama kwa imani wakati ujao ambao hauna migongano tena na  mantiki zilizopita. Ni wakati ambao utajikita katika upendo wa pamoja (Rm,13,8). Ni wakati ambao wote tunaalikwa kuchagua zawadi zitokazo kwa kila tamaduni tofauti za kidini na kupokea na kukubali kama urithi wa pamoja. Kabla ya mvutano,utofauti na majeraha yaliyopita, Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa ipo hali halisi ya wakati uliopo yaani ya umoja unajikita katika msingi wa kudumu  wa ubatizo wetu.

 Ubatizo umetufanya sisi sote kuwa wana wa Mungu na ndugu kati yetu. Na kwa njia hiyo haiwezekani tena  kuruhusu uadui uingilie kati. Iwapo wakati uliopita hauwezekani kuubadili, basi wakati ujao unatualika,  kuwa haiwezekani kurudinyumba, na hiyvo sasa ni kutatufa kuhamasisha kwa nguvu umoja na katika upendo na imani. 

Tunaalikwa  pia kukesha mbele ya majaribu yanayojitokeza katika safari yetu ndefu. Katika maisha ya kiroho kama yake maisha ya Kanisa, iwapo unasimama ni kurudi nyuma , kwasababu ya kuridhika, kuwa na hofu, uvivi , uchovu au mambo mengine yanayojitokeza wakati wa safari kuelekea kwa Bwana na ndugu zke. Baba Mtakatifu anawalika kujikita zaidi katika kujibu, hasa kutazama maskini na ndugu wadogo wa Bwana (Mt 25,40).

Hizo ndizo ishara msingi katika safari yetu tunazohimizwa, na itakuwa vizuri zaidi kugusa majeraha kwa nguvu ya uponyaji, katika uwepo wa Yesu kwa njia ya dawa ambayo ni huduma yetu. Na ili iweze kutimilizika kuwa na umoja,  ndiyo safari ambayo tunaitwa kwa jina la Yesu. Lakini  bado kuna siku nyingi za kuteseka kwasababu ya kutoa ushuhuda wa Yesu. 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.