2017-11-30 16:52:00

Papa:Ujumbe wa Papa kwa maadhimisho ya miaka 20 ya "A Sua Immagine"!


Ninyi ni vijana mliojaa furaha, na utendaji wenu huchanua ubunifu mpya kwa lika la vijana, siku zote mkiziba mianya inayotaka kuleta woga,  wasiwasi na mashaka katika maisha ya vijana. Ni pongezi za Baba Mtakatifu Francisko kwa Waandaaaji na Watangazaji wa Kipindi cha Televisheni chenye jina “ Kwa Sura Yako” “A Sua Immagine “ ambacho hutolewa na Televisheni ya Italia,( RAI).

Papa  ametaja kipindi cha “A Sua Immagine “, kilichoanzishwa mwaka 1997,  kuwa ni njia mpya ya kufikisha Habari Njema ya Injili kwa wakazi wa Italiana dunia kwa ujumla.  Ameitaja kuwa huduma ya thamani sana yenye kufikisha Neno la Mungu katika kila kaya ,pamoja na shuhuda za waamini wanaoishi katika  maeneo ambako kuwa Mkristo linakuwa ni kosa kubwa linalositahili hata kifo.

Pongezi za Papa, zinaendela kuishukuru RAI, kwa  kila Jumapili , kuweka nafasi ya Ibada na sala ya adhuhuri ya Malaika “Angelus,  hasa akiwafikiria wagonjwa na wazee au watu wenye udhaifu wa mwili,  ambao hawawezi kufika makanisa kusikiliza Neno la Mungu au kushiriki moja kwa moja katika Ibada za Misa au kusikiliza ushuhuda zinazotolewa na waamini wengine, waliotawanyika sehemu zote za dunia, ambao hupambana na kila aina ya matatizo kutokana na Imani yao kwa Kristo Msulubiwa. Au, wale wanaotoa maaelezo yao kwa miujiza midogomidogo inayotokea kwa kulimwilisha Neno la Injili katika maisha.

Papa akitafakari kipindi cha miaka ishirini iliyopita ya  uwepo wa kipindi hiki, amehimiza waandaaji kutafakari kwa kina zaidi nini cha kuongeza au kupunguza katika mahitaji ya wasikilizaji wao na hasa akiwafikiria vijana au wale wasiokuwa na sauti katika jamii ambao sauti yao haisikilizwi.  Hivyo amewataka wanahabari wabebe  vyombo vyao hadi vitongojini bila kuchoka , kupeleka Neno la Injili hadi ijulikane kwamba,  Injili si maandishi ila ni maisha yanayotakiwa kumwilishwa katika utendaji wa  kila siku.

Kipindi hiki cha “A Sua Immagine “ni matokeo ya ushirikiano wa pamoja kati ya Rai na Baraza la Maaskofu Katoliki la Italia na hufanikishwa na kikundi cha watalaam katika mawasiliano wenye kuwa na mapenzi makubwa katika utoaji wa kipindi hiki.

Thabita J. Mhella
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.