2017-11-29 16:37:00

Mkuu wa Baraza Kuu la Wabudha ametoa wito wa Mshikamano na ujenzi wa madaraja


Msingi wa kwanza wa kila dini unajikita juu ya upendo  wa dhati na  kwa wema, ambapo inahitajika kushirikiana kwa pamoja kwa wema wa familia na uzalendo wa raia ili kuweza kudumisha amani ya chi kwa maana juhudi za amani ya kudumu inawezekana katika mataifa ya sayari hii. Ni maneno ya Mwenyekiti wa Kamati ya  Sagha ya Wamonaki Wakibudha  Bhaddanta Kumarabhivansa wakati wa ufunguzi wa mkutano na Baba Mtakatifu Francisko  katika kituo cha Kaba Aye Yangon.

Katika hotuba yake  mwenyekiti wa kibudha, anasema, kiukweli pamoja na madhehebu kukiri dini tofauti lakini wote wanapitia njia moja ambayo inapelekea ustawi  wa binadamu. Pia anaongeza kusema, anaamini kuwa imani zote za dini zinaweza kupeleka kwa namna moja au nyingine ustawi wa amani na matarajio mema, maana ndiyo msingi mkuu ulio wafanya wakusanyike kwa pamoja na tofauti za imani zao za kidini.

Aidha anasema, katika ulimwengu wa sasa, inatishia kuona matendo ya ugaidi na itikadi kali ambazo zinafanyika kwa jina la dini , kwa njia hiyo anaongeza, kutokana na dini zote kuwa na mafundishi ya wema wa binadamu haiwezekani kukubali matendo ya kigaidi na itikadi kali  zinaleta vurugu za imani ya kidini. Anasisitiza kuwa  hiyo ni kutokana na kuamini  kwa dhati kuwa, ugaidi na utikadi kali zinatokana na tabia mbaya ya kutafsiri mafundisho asili ya dini zao,  maana wafuasi wengine walioanzisha makundi hayo mara nyingi wanatengua tafsiri kutoka katika mafundisho asili kutokkana na  msukumo wa utashi wao, hisia, hofu na kukata tamaa vitu vinne ambavyo ni vizingiti katika mawazo ya waanzilishi wa itikadi kali.

Watu wote duniani ni lazima kushirikiana na kujikita kwa pamoja bila woga ili kutimiliza mshikamano wa maisha kijamii kwa usalama na ulinzi wa dunia. Kwa njia hiyo anasisitiza kuwa  inawezekana kupinga aina zato zinazochochea chuki, uongo , migogoro, vita na maandamano na kushutumu vikali kwa wale wanaojikita katika shughuli hizi. Kama viongozi wa dini duniani ni lazima kuwa wajenzi yakinifu wa umoja na mshikamano wa jamii ya kibinadamu kwa kufuata kila mmoja mafundisho msingi ya dini yake na kuongeza nguvu zaidi kwa ajili ya amani na usalama wa dunia.

Aidha amaesema, ni lazima kujenga kati yao maelewano, heshima na imani thabiti ili kuweza kufikia amani kamili ambayo ni matarajio ya jamii ya kibinadamu. Hivyo ndiyo kazi kubwa kwa waanachama wa imani tofauti ambao pia wanaalikwa kushuhudia wakiwa mstari wa mbele, kuwa wajenzi wa madaraja ya amani, duniani. Wao kama wamonaki wa kibudha mawazo yao ya kitasaufi, tamaduni na dini wanatambua kuwa ni msingi, ni wajibu wao kwa kila mtu kuongea wazi wakupinga kila aina ya upotofu wa dini. Aidhawanaamini kabisa kuw,a watu wote wenye imani tofauti, wanaweza kutimiza malengo yaliyokubaliwa  kwa nyakati zijazo katika ulimwengu tunaoishi kwa amani endelevu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.