2017-11-28 16:10:00

Papa:Utofauti wa dini usiwe chanzo cha migogoro, ni nguvu ya umoja wa nchi!


Baba Mtakatifu Baada ya kukutana na Rais wa nchi, Htin Kyaw, Mshauri Mkuu wa Rais Bi Aung San Suu Kyi na Waziri wa Mambo ya nchi za nje, umefuatia Mkutano wa kwa viongozi wote wa nchi, raia na wanadiplomasia, katika jengo moja kilometa chache kutoka katika makao makuu ya Rais wa nchi hiyo.  Na katika hotuba rasmi ya kwanza, Baba Mtakatifu amesema kuwa, amemefika kuimarisha imani ndogo tu, lakini yenye chachu katika jumuiya ya wakatoliki wa nchi na kuwatia moyo katika  hali ngumu  wanayokabiliana nayo wakitoa mchango  wao kwa ajili ya wema wa nchi, lakini pia anapendelea kwamba, ziara hiyo ieleweke kuwam ni kutaka kuwakumbatia watu wote wa nchi kwa kutoa neno la kuwatia moyo wote ambao wanajikita katika kazi ya ujenzi wa haki za kijamii, mapatano na kwa waliobaguliwa.

Nchi ya Myanmar anasema, imebarikiwa kuwa na zawadi muhimu ya uzuri, hata kuwa na mali asili, lakini mali kubwa ni tunu na thamani ya watu wnyewe, ambao wamateseka na wanaendelea hata leo kuteseka kwa sababu ya migogoro ya ndani kwa ndani na vizingiti ambavyo vimedumu kwa muda mrefu vikasababisha migawanyiko ya kina. Pamoja na kwamba nchi hadi sasa inajikita katika kurudisha amani, Baba Mtakatifu anaongeza, uponyaji wa majeraha haya ndiyo chachu msingi ya  kuweka kipaumbele kwa sera za kisiasa na kitasaufi.

Aidha anawapongeza juhudi kubwa ambayo serikali imejikita kwa maana ya kusistiza mchakato wa ujenzi wa amani na mapatano katika nchi. Lakini bado wanapaswa waendelee kutia juhudi kubwa kwa ajili ya amani na kuheshimu haki za binadamu. Ametaja hata kuhusu Hati za Kimataifa ya haki za binadamu zilizotangazwa na Umoja wa Mataifa kuhusiana na uhamasishaji haki katika ulimwengu, amani, maendeleo na kwa ajili ya kutafuta suluhisho la migogoro kwa njia ya mazungumzo bila kutumia nguvu.

Na kwa njia hiyo anasema, wakati endelevu wa nchi ya Myanmar lazima uwe wa amani, na amani inayoheshimu hadhi ya binadamu,  haki ya kila mtu katuka jamii, kwa kuzingatia kila kikundi cha kabila, uzalendo wake na heshima zake, haki zake zinazomwezesha kujieleza katika kikudi na kwa kila mtu bila ubaguzi kwa ajli ya kutoa mchango kwa wema wa wote.

Katika changamoto hiyo, Baba Mtaktifu anaendelea, dini zote zina fursa ya pekee kuwa wawakala katika kusaidia  kuondoa sababu za migogoro na kujenga madaraja kwa njia ya mazungumzo, kutafuta haki halikadhalika  kuwa sauti ya kinabii kwa wote wanaoteseka. Utofauti wa dini Baba Mtakatifu amesema usiwe ni sababu na vyanzo vya migawanyiko au kutoaminiana, badala yake iwe ni nguvu kwa ajili ya umoja , msamaha, kuvumiliana na heshima kwa ajili ya kujenga nchi.

Dini zinaweza kuwa ni fursa nyeti anafasi katika kuponyesha majeraha , kiroho na kisaikolojia kwa wale ambao kwa miaka mingi wameishi katika mateso. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anaonesha jinsi gani dini zote zinaweza kuwa ishara ya matumaini kwa kujikita kwa udhani zaidi katika shughuli nyeti kwa viongzo wote wanaoongoza vikundi vya makabila na tamaduni tofauti zilizomo katika nchi kwa ajili ya ujenzi thabiti wa amani na msaada wa maskini, elimu ya dhabiti ya kuonesha thamani ya dini na kibinadamu.

Baba Mtakatifu anamalizia akisema kuwa ni katika thamani hizi ndipo ujenzi wa maisha ya baadye yanaweza kuonekana , kwa maana ya umuhimu wa kuwekeza mafunzo kwa vijana, uaminifu, ushirikishwaji na mshikamano kama msingi wa demokrasia na ukuaji wa umoja na amani kwa ngazi zote kijamii.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.