2017-11-28 11:20:00

Papa na viongozi wa madhehebu ya kidini Myanmar:umoja katika utofauti!


Tarehe 28 Novemba 2018 katika ziara ya Baba Mtakatifu itakuwa nikufanya  mikutano rasmi, baada ya mapumziko ya safari yake. Baba Mtakatifu Francisko amekutana na viongozi wa Dini katika makao ya Askofu Mkuu huko Yangon, saa 4.00- 4.30  saa za Ulaya. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa chakula ambapo ametoa hotuba yake bila maandiko kwa lugha ya kihispania. Kiini cha mazungumzo yake, yamehusu mada juu ya umoja katika utofauti.

Katika lugha ya kishipania kwa viongozi wa madhehebu ya kidini ya myanmar, Baba Mtakatifu amezungumza na  wabudha, waislam, wahindu, wayahudi, wakatoliki na wakristo wa makanisa mengine. Mkutano umechukua muda kama dakika 40, hivi ambapo ameongozwa na  zaburi isemayo jinsi gani ilivyo vya kuishi kwa pamoja kama ndugu na kuongeza susema kuwa, ndugu si maana ya kufanana. Umoja siyo sale ya shule na  hata katika dhehebu moja ndani yake hawafanani, kwa maana kila mmoja anayo thamani yake, utajiri wake, hata udhaifu wake.

Sisi wote ni tofauti na kila dhehebu lina utajiri wake, utamaduni wake wa kushirikishana.  Lakini hiyo inawezekana tu kwa yule anaiyeishi na amani. Na amani inajengwa katika mkusanyiko wa kwaya ya utofauti hivyo umoja daima unatokana na utofauti! Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na mazungumzo yake bila kuseoma, amesema, amani ni uelewano, hasa sasa katika kipindi cha  uzoefu wa tabia za kidunia ya kupendelea usale yaani ya  , kutaka kila kitu kifafane. Lakini hiyo inaua ubinadamu! Anasisitiza Baba Mtakatifu. Hiyo ndiyo kusema ni  ukoloni wa kitamaduni.

Ni lazima kutambua utajiri wa tofauti zetu (kama vile kabila dini, watu) na utofauti huo unatoa mazungumzo. Ni katika tofauti hizo unaweza kujifunza kutoka kwa mwingine kama ndugu. Baba Mtakatifu anatoa wito hasa wa kuishi kama ndugu ili aweze kusaidia kujenga nchi yao ambayo kijiografia inaonesha utajiri mwingi na utofauti nyingi. Asili ya nchi ya Myanmar ni yenye utajiri mkubwa wa utofauti, kwa njia hiyo hawapaswi kuwa na hofu ya tofauti! Amethibitisha.

Baba ni mmoja na wote ni ndugu, hivyo wabaki  kama ndugu! Aidha  amewashuri kuwa, inapotokea mizozano kati yao, ifanyike kwa utambuzi kuwa ni ndugu kati yao na kupatana  kwa haraka. Ni kubaki  kuwa ndugu  daima . Na ndiyo yeye binafsi anafikiria kuwa  huo ni mtindo wa wa kujenga amani.
Amamemalizia Baba Mtakatifu na wito wa ujenzi wa amani akisema, wao wasiache waundwe na  ukoloni wa utamaduni  kwa maana uungwana wa kweli wa Mungu ni ule unaofanywa kupitia tofauti na tofauti ni utajiri wa amani! 

Hata hivyo taarifa zaidi zinaonesha kuwa mara baada ya kufika na chereko chereko za watu kumpokea katika msafara alipumzika na jana jioni, maasa yaliyofuatia huko Myanmar, saa kumi na mbili alipata kuongea na Mkuu wa  majeshi ya Birmania, Jenerali Ming Aung Haling katika makao makuu ya Askofu Yangon ni mkutano uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 30 Novemba 2017. Na habari kutoka Vatican pia zinasema kuwa,huyo ni kiongozi mwenye majukumu makubwa na madaraka ya nchi kwa kipindi hiki.

Ratiba ya mchana: Baba Mtakatifu atakwenda na ndege Nay Pyi Taw, mji Mkuu wa Mynamar, mahali ambapo atakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Birmania na mshauri wa nchi mtuzwa Nobel ya amani Aung San Suu Kyi, ambapo baadaye atahutubia wananchi.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.