Ili kuweza kuendelea na Katekesi juu ya Misa, tunaweza kujiuliza: msingi wa misa ni nini?: Misa ni kumbukumbu ya Fumbo la Pasaka ya Kristo. Hiyo inatufanya tushiriki ushindi dhidi ya dhambi na kwa kuleta maana kamili ya maisha yetu. Ni maneno katika utangulizi wa Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 22 Novemba 2017 katika viwanja vya Mtakatifu Petro mjini Vatican katika mwendelezo wa sehemu ya tatu, kuhusu mada ya maadhimisho ya Misa Takatifu.
Ili kutambua thamani ya Misa, hawali ya yote ni lazima kutambua maana ya “kukumkumbu” kibiblia. Hiyo siyo tu kukumbuka matukio yaliyopita, bali uhakika kwa namna ya wakati uliopo na kufanya kukumbukumbu kwa kile kilichotendeka karne ishirini ziliyopita. Ni kwa namna hii Israeli anatambua ukombozi wake toka misri: Kila mara Pasaka inapoadhimishwa, matukio ya kutoka hufanywa yawepo katika ukumbuko wa waamini ili yalingana na maisha yao. (Katekisimu ya Kanisa Katoliki 1363).
Kwa njia ya mateso, kifo ufufuko na kupaa mbingu kwa Yesu Kristo umetuletea ukamilifu
wa Pasaka. Misa ni kumbukumbu ya Pasaka yake, ya kutoka kwake ili kuleta ukamilisho
wetu sisi na kufanya tuondokane na utumwa wa dhambi ,tupate kuingia katika ahadi
ya ufalme wa Mungu.
Ekaristi daima itatupeleka katika upeo wa juu zaidi kutokana na matendo ya ukombozi
wa Mungu: Bwana Yesu ambaye aliumega mkate kwa ajili yetu na kumimina juu yetu huruma
yake na upendo wake alioonesha akiwa msalabani hivyo kuupyaisha moyo wetu, kuishi
kwetu na namna yetu ya kuhusiana na Yeye na ndugu. Baba Mtakatifu anasema, Mtaguso
wa Pili wa Vatican unasema: Kila mara inapofanyika sadaka ya msalabani ambayo ni Yesu
Kristo kondoo wa Pasaka yetu aliyechinjwa, na kuadhimishwa juu ya altare, ni kufanya
tendo la ukombozi (Cost. dogm. Lumen gentium, 3).
Kila adhimisho la Ekaristi ni mwonzi wa jua bila usio kuwa na mawio yake ambaye
ni Yesu Kristo. Kuudhuria Misa kwa namna ya pekee siku ya Jumapili, Baba Mtakatifu
nathibitisha, maana yake ni kuingia katika ushindi wa Mfufuka, kuangazwa na mwanga
wake pia na kupashwa joto kale. Kwa kuadhimisha Ekaristi na Roho Mtakatifu, inatufanya
kushiriki maisha matakatifu ya Mungu ambaye ana uwezo wa kubadilisha kila mtu na utu
wetu wa kufa.
Hatua za mchakato wa kutoka kifo kufikia maisha mapya, na kipindi cha umilele Bwana
Yesu anatusukuma hata sisi katika hatua zake ili kufanya naye Pasaka. Katika Misa
tunaungana naye. Kwa maana, hakika Yeye anaishi nasi na sisi tunaishi naye kama anavyothibitisha
Mtakatifu Paulo kuwa:“Maana mimi kwa njia ya sheria naliifia sheria ili nimwishie
Mungu. Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo
yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana
wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu”.( » (Gal 2,19-20).
Damu yake inatupa uhuru ikiwa na maana ya uhuru wa kifo na hofu.Tunapata uhuru na si wa kimwili tu lakini pia kifo cha kiroho ambacho ni ubaya, dhambi ambazo mara nyingi tu waathirika, hata kuwasababishaia wengine. Kwa njia ya dhambi maisha yetu yanachafuka na kupoteza uzuri na maana yake ya kuchanua. Badala yake Kristo ni ukamilifu wa maisha, tangu ashinde kifo na daima. Kanisa linathibitisa wakati wa maadhimisho ya Misa kuwa, kwa ufuko wake alivunja vunja kifo na kukuunda maisha mapya. Pasaka ya Kristo ni ushindi wa maisha dhidi ya kifo, maana yeye alibadili kifo kwa kwa njia ya upendo upeo. Katika Ekaristi, Yeye anataka kueleza upendo huo wa Pasaka yaani ushindi. Iwapo tunapokea kwa imani, nasi pia tunaweza kupenda kweli Mungu na jirani na kupenda kama yeye alivyo penda sisi kwa kutoa maisha yake.
Iwapo upendo wa Kristo huko ndani mwetu, tunaweza kutoa upendo mkamilifu kwa mwingine, aidha kuwa na uhakika wa kina ya kwamba hata kama jiarani yangu atanikwaza siwezi kukwazika naye kabisa. Baba Mtakatifu ametoa mfano kuwa, wafiadini walitoa maisha yao wakiwa na uhakika wa ushindi wa Kristo dhini ya kifo. Ni kwa njia ya uzoefu wa nguvu ya Kristo na nguvu ya upendo, Nasi kweli pia tunao uhuru na kujitoa bila kuwa na hofu. Akitoa mifano kadhaa , amesema,tunapoingia katika misa ni kama vile tunakwenda njia ya msalaba, ndiyo fursa ya kutafakari Kalvario, na kutambua Yesu ni nani. Pamoja na hayo ametoa swali, je ni mara ngapi inatokea kujiuliza kipindi hicho, badala ya kuzungumza na kupiga picha, au kama vile kidogo kufanya tamasha na maonesho?
Hilo silo jambo zuri Baba Mtakatifu amesisitiza kwa mara nyingine kuwa, ndani ya misa yupo Yesu, lazima kubaki kimya,hata kulia, hata furaha za kukombolewa. Ni lazima kufikiria hayo tunapoingia katika misa: ninaingia katika njia ya Kalvario mahali ambapo Yesu alitoa maisha kwa ajili yangu. Na kwa namna hiyo mambo ya kufanya tamasha yanapotea, hata mazungumzo yanayo tuondolea umakini katika kuadhimisha jambo jema ambalo ni Misa na Yesu Kristo mshindi. Amemalizia na mawazo kwamba sasa imekuwa wazi jinsi gani Pasaka ipo hata leo hii inafanya kazi kila wakati tunapoadhimisha Misa, kwa maana ya kufanya kumbukumbu. Kushiriki Ekaristi tunaingia katika fumbo la Pasaka ya Kristo na kutupatia uwezo wa kupitia kifo na Yeye ili kuingia katika maisha.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |