2017-11-21 15:26:00

Papa:Ukoloni na utamaduni wa kikoloni hauna uvumilivu ndipo unatesa waamini


Ukoloni na utamaduni wa kikoloni haukubali uvumilivu na ndipo huishia  hata kuwatesa waamini pia. Ni maneno yaliyomo katika mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko asubuhi ya tarehe 21 Novemba katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican mahubiri yake yaliyojikita juu ya mfiadini Eliezer aliye tajwa katika somo la kwanza la Makabayo (mak 6,18-31).

Akifafanua zaidi kuhusu somo la kwanza, Baba Mtakatifu anaeleza: kuna aina tatu msingi za mateso: ya kwanza kuteswa kwa ajili ya dini kwa mfano vita vya miaka ya 30 au vita vya usiku wa Mtakatifu Bartolomew, nyingine ni Vita  vya dini au kisiasa;  aina ya tatu ya kuteswa ni  ile ya kijamii ambayo ni aina mpya itokanayo ubaguzi wa kutaka kufanya kila kitu kipya au kusafisha uwanja wa mila, wa utamaduni na hata katika dini za watu. Ka njia hiyo, ina ya tatu ya kuteswa ndiyo aliyokumbana nayo Eliezer, akahukumiwa afe kwa ajili ya uaminifu kwa Mungu.

Baba Mtakatifu anagusia historia ya kuteswa kwa tamaduni kuwa, ilianza tangu  jana katika kitabu cha Makaboyo, wakati watu wanafurahia uchipukizi wa dhambi katika utawala wa Antioko.  Antioko Epifani walikuwa wamefikiria kufanya agano jipya, na ambapo walikwenda kwa mfalme ili waanzishe kitengo kipya  cha kipagani katika nchi. Hayakuwa ni mawazo au miungu bali taasisi, anasema Baba Mtakatifu. Hadi kufikia watu hao kukua katika Sheria za Bwana na kufanya waingize utamaduni mpya yaani taasisi mpya ambayo inafanya kusafisha kiwanja kwa yote ikiwa ni pamoja na  utamaduni, dini na sheria.

Kila kitu kipya na upyaisho ndiyo kusema ni ukoloni kwa kweli wa kiitikadi ambazo zinawalazimisha watu waisraeli wawe na tabia hii moja, yenye msingi kwamba kila kitu kinachofanyika lazima ndiyo hicho nana hakuna uhuru wa mambo mengine.
Wengine walikubali kwa maana walifikiri ni jambo jema ili weweze kuwa kama wengine na kwa njia hiyo wakatoa tamaduni na watu wakaanza kuishi kwa namna nyingine. Lakini ili kuweza kuwa na taasduni za kweli za watu, ulizuka upinzani ambapo Eliezer,  mtu mkarimu na mwenye heshima kama kitabu cha makabayo kinavyoeleza historia yake ya ushahidi na mashujaa. Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa  mateso kutokana na ukoloni wa kiitikadi daima umeendelea hivyo kuharibu , na kutaka kufanya kila kitu kifanane , hakuna uwepo wa kuvumila utofauti.

Eliezer, alikufa akifikiria vijana kwa kuwaachia mali kwa mfano maisha anayotoa kwa upendo wa Mungu, sheria inayotoa mzizi ya wakati ujao ,lakini kutokana na mizizi iliyotanda inayozaa ukoloni wa kitikadi na utamaduni, bado kuwa mzizi mwingine unaotoa maisha ili kufanya ukue wakati uliopita.
Baba Mtakatifu anatoa onyo kuwa mfalme wa Antioko ulikuwa wni utawalwa mpya lakini mbaya kwa kuona hilo ni lazima kufikiria Injili ambayo ni Yesu mwenye huleta upya na lazima kujua kutofautisha kati ya habari njema inayotoka kwa Mungu na zile itikadi tofuati. Lakini ni lazima kuchagua mapya : na ndiyo hanari mpya ya Bwana inayotokana na Roho Mtakatifu. Zamani ilikuwa dhambi kuua watoto lakini leo hii wanaua watoto: Jana kulikuwa na utofauti  ambayo Mungu alifanya? Kulikuwapo na kuheshimu kazi ya uumbaji, lakini leo hii ni kutaka kufanya mapya na kuchanganya mambo yote Papa anasema. Lakini Habari mpya  na njema ya Mungu ni ile ya mchakato wa  kukua na kutazama hata wakati ujao.

Lakini ukoloni wa kitiikadi na utamaduni, unatazama tu wakati uliopo na kukataa yaliyopita bila kutazama yale yajayo. Ni kuishi kwa wakati na siyo kwa kipindi kirefu, ndiyo maana huweza kutoa ahadi ya kitu chochote cha wakati ujao. Tabia hiyo ya kufanya kila kitu kinafanane na kufuta tofauti ni dhambi kubwa ya kupinga kazi ya uumbaji ya Mungu. Kila inapojitokeza ukoloni mpya wa kiitikadi  unatenda dhambi dhidi ya Mungu muumbaji kwasababu ya kupenda kubadilisha kazi yake ya  uumbaji aliyoifanya. Matendo hayo yamejitokeza kwa kipindi kirefu cha kihistori ambacho lakini kimepata dawa yake ambayo ni  kwa njia ya ushuhuda yaani mashahidi.

Eliezer, ni shahidi wa maisha, ni mfano wa kuigwa . Eliezer hakufikiria fedha bali lifikiri wakati ujao kwa urithi wa ushuhuda kwa vijana unatoa ahadi ya matunda. Kutokana na ushuhuda huo unakuwa ni mzizi ya maisha kwa ajili ya wengine,  ndiyo maana Baba Mtakatifu anamalizia akitoa wito wa kuiga mfano hasa kipindi hiki cha kuchanganyikiwa kwenye ukoloni wa utamaduni, kitasaufi unaotolewa na kuwa kichocheo cha vishawishi.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.