2017-11-17 15:48:00

Papa amekutana na Rais wa Austria Bwana Alexander Van der Bellen


Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Austria Bwana Alexander Van der Bellen katika Nyuma ya Mkutano Vatican tarehe 16 Novemba 2017.  Baada ya mkutano huo pia amekutana na Kardinali Pietro  Parolin Katibu akisindikizwa na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Wakati wa mazungumzo yao wameonesha uhusiano mzuri na ushirikiano  uliopo kati ya Vatican na nchi ya Austria. Pamoja na hayo wamesisitiza juu ya mambo muhimu ya maisha hasa ya ulinzi wa hadhi ya maisha ya binadamu, kuhamasha utamaduni wa makutano na kukuza ari ya utunzaji wa mazingira.
Na mwisho wanaonesha nafasi ya Jumuiya ya Kimataifa katika kutafuta suluhisho ya amani katika migogoro iliyopo katika kanda nyingi  za dunia na kusisitiza juu ya wajibu wa pamoja kwa ajili ya dunia ilisiyokuwa na silaha za kinyuklia.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.