2017-11-16 16:35:00

Papa amepewa zawadi ya gari ambalo litawekwa mnadani kwa ajili ya wahitaji


Zawadi ya gari mpya yenye thamani kubwa aina Lamborghini Huracan  imetolewa asubuhi ya tarehe 15 Novemba 2017 kwa Baba Mtakatifu Francisko, wakiwapo wakuu wa Kampuni ya Magari kutoka  mji wa Mtakatifu Agata Bologna nchini Italia. Katika uwanja wa Mtakatifu Marta, Baba Mtakatifu ameweka saini yake mbele ya mlango wa gari hilo, ambalo litawekwa kwenye mnada wa Sotheby’s  na fedha zitakazo patikana zitawakililishwa moja kwa moja kwa Baba Mtakatifu kwa ajili ya matendo ya upendo kwa baadhi ya  Vyama ili kusaidia mahitaji ambavyo Papa mwenyewe ameelekeza kama ifuatavyo:

Sehemu ya fedha hizo zitakwenda kusaidia ujenzi wa Vijiji vya Bonde la Ninawi, kwa njia ya Chama cha Kipapa cha Kanisa Hitaji. Mpango huo unataka kuwasaidi wakristo wa Bonde la Iraq waweze kujenga au ukarabati majengo ya umma na majengo ya kusali. Baada ya kukaa miaka mitatu wamesongamana huko Kurdistan Iraq mwishowe wakrsto hao wanaweza kurudi katika mizizi yao na kupata hadhi yao.

Sehemu nyingine ya fedha itakayo patika katika uuzaji wa gari hilo itasaidia Jumuiya ya Papa Yohane XXIII ambao wanasaidia wanawake waathirika wa biashara ya utumwa na ukahaba (mpango wa Nyumba ya Papa Francisko). Ni tukio linalojitokeza katika maadhimisho ya miaka kumi tangu kifo cha mwanzilishi wa Jumuiya hiyo Padre Oreste Benzi, wakati huo huo mwaka 2018  sambamba na  miaka 50 tangu kuanzisha jumuiya hiyo  na pia sehmu nyingine ya fedha itatumika kwa ajili ya vyama viwili vya Italia vinavyojikita zaidi na shughuli za kitume Afrika (Gicam cha Professa Marco Lanzetta, Daktari Bingwa na pia chama cha Rafiki wa Afrika ya Kati, ambacho kwa miaka mingi wanasaidia mipango hasa kwa ajili ya wanawake na watoto.

 Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.