2017-11-16 16:13:00

Ni Roho Mtakatifu anafanya Ufalme wa Mungu ukue na si mipango kichungaji!


Ufalme wa Mungu siyo tamasha, au sherehe za  Carneval, siyo matangazo ya biashra: ni Roho Mtakatifu anaye fanya Ufalme wa Mungu ukue, na si katika mipango mikubwa ya kichungaji. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko kwenye mahubiri ya Asubuhi ya tarehe 16 Novemba katika Kanisa la Mtakatifu Marta  mjini Vatican mahali ambapo anatafakari  Injili ya Mtakatifu Luka 17,20-25) kuhusu ufalme wa Mungu. Katika mahubiri yake anaanza na maswali ya mafarisayo wakiuliza kuwa ufalme wa Mungu utakuja lini?

Lakini kuna wakati mwingine swali linalokuja kwa nia nzuri au la... , mara nyingi katika Injili kwa mfano, Mtakatifu Yohane Mbatizaji alipokuwa gerezaji kwa uchungu, akawatuma mitume wake  wakamuulize Yesu kama kweli ndiye walikuwa wakimsubiri. Au katika swali jingine "kama ni wewe Yesu basi shuka msalabani"... Baba Mtakatifu anaongeza, daima upo wasiwasi, au utukutu wa kutaka kujua juu ya ufalme wa Mungu utakuja lini.
Yesu mwenyewe amejibu kuwa, ufalme wa Mungu u kati yao na ndiyo habari njema katika Hekalu la Nazareth, mahali  ambapo Yesu alichukua kitabu na kusoma Maandiko ya Isaya na kusema "Leo hii imetimia kile kilichoandikwa "

Kama mbegu inayo pandwa na kukua ndani yake, ndiyo  kama ufalme wa Mungu unavyokua kimya kwa kujificha kati yetu . Ni ufalme inaojificha kama vile tunu au dhahabu lakini daima ufalme unakuwa kwa unyenyekevu. Ni nani anayefanya mbegu ikue na kutoa maua yake? Ni Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu aliye ndani yetu, ni roho ya upole, unyenyekekevu, utiii na urahisi. Ni Mungu  anayefanya ukue ufalme wake na siyo kwa njia ya mipango mikubwa ya kichungaji, ni roho iliyofichika ambayao inakua na kufikia kutoa matunda. Hata hivyo anaongeza, ufalme wa Mungu daima ni zawadi ya mshangao, inakuja  kwa ghafla bila kutegemea. Kwa njia hiyo ufalme wa Mungu haufanya matangazao na kujinesha mimi ndiyo la! kwa maana si tamasha na mbaya zaidi kufikiria kama sherehe za carneval.

Na ufalme wa Mungu hauwezi kuonekana katika ukiburu na ufedhuli, kwa maana hauhitaji matangazo. Ufalme wa Mungu umefichika kwa unyenyekevu na  unakua. Ametoa mfano wa Mama Maria aliyekubali kuwa mama wa Mungu kwa unyenyekevu. Alipokuwa chini ya msalaba, alisikia hata maneno ya mabaya uwenda kwamba ni mama wa mtoto mwalifu, lakini alikuwa pale kwa unyenyekevu

Sisi wote tunaalikwa kutengeneza njia ya uUlme wa Mungu kwa maana ni wito, ni neema na zawadi ya bure maana  hainunuliwa, ni neema ambayo Mungu anaitoa bure . Ni neema kwa wabatizwa wote kwa njia ya Roho Mtakatifu. Tuombe Roho Mtakatifu aweze kukuza ndani mwetu na Kanisa nguvu na mbegu ya Ufalme wa Mungu ili uweze kuongezeka  na kuwa makimbilio ya watu wengi kwa kutoa matunda ya utakatifu

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.