2017-11-11 17:15:00

Papa ametuma ujumbe kwa Mkutano wa Kitaifa wa Vituo Vya msaada wa maisha


Umezinduliwa huko Milano nchini Italia, Mkutano wa 37 wa Taifa wa Vituo vya Msaada wa Maisha. Katika tukio la Mkutano wa Kitaifa wa Vituo vya msaada wa Maisha, Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake, ulio tiwa saini na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin ukilekezwa kwa Kardinali Bassetti Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Italia.

Ujumbe huo unawasalimia wote na kuwasifu kwa shughuli nyeti  wanayo endeleza hasa  ya kutetea na kuhamasisha na kukuza  maisha ya kibinadamu.Ni matumaini yake kuwa Mkutano wao unaweza kuwasaidia zaidi katika kutafakari kwa kina juu ya thamani ya maisha ya binadamu na kupokea hali halisi ya zawadi ya Mungu isiyokuwa na kipimo katika utajiri wake wa kiajabu. Na mwisho hakosi kuomba sala kwa ajili ya huduma yake kwa Kanisa na kuwatakia Baraka za Mungu hasa za roho Mtakatifu kwa wote wanaoshiriki katika Mkutano huo.

Katika uzinduzi wa Mkutano huo naye  Mwenyekiti wa Chama cha Kitaifa cha Vituo Msaada wa Maisha, Bwana Gian Luigi Gigli ameonesha changamoto zilizopo  mbele ya binadamu wa sas ana hasa zile za  ukosefu wa kuhakikisha hadhi ya binadamu na heshima ya maisha yote ya kibinadamu. Amesema kuna ongezeko kubwa zaidi la ukosefu wa kuheshimu na kujali binadamu na mazingira kwa ujumla, na hivyo amewaalikwa wote kupokea kwa ari zote ushauri na wito wa Baba Mtakatifu Francisko anaye hamasisha juu ya ulinzi kwa ujumla wa maisha ya binadamu mbele ya kufumbia macho na utofauti katika dunia hii.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.