2017-11-03 10:50:00

Sala ya Papa mbele ya Makaburi ya Wayahudi huko Ardeatina Roma


Bwana wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo  (Kut 3,6). Umejionesha kwa majina hayo ulipomtokea Musa kwa ajili ya kuwakomboa watu wako kutoka utumwani Misri.Mungu wa Ibrahimu,Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo: Mungu anayefanya agano la binadamu, Mungu anafanya kifungo cha upendo mwaminifu daima.

Wewe ni mwenye huruma na mwema kwa kila mtu na kwa watu wote wanaoteseka."Nimetazama shida za watu wangu na kusikia kilio chao,ninatambua mateso yao" (Kut 3,7). Mungu mwenye sura na majina. Mungu wa kila binadamu wa 335  waliouwawa tarehe 24 Machi 1944, mahali ambapo masalia yao yapo katika makaburi haya. Wewe unatambua sura zao na majina yao. Unatambua wote hata wale kumi na mbili wasio julikana majina yao kwa maana hakuna anaye sahaulika mbele yako.

Mungu wa Yesu na Baba Yetu  uliye mbinguni. Kwa Neema yako Yeye  amefufuka na sisi tunakutambua  jina lako kuwa ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo. Hiyo ina maana kwamba wewe siyo Mungu wa waliokufa bali walio hai (Mt 22,32), na agano lako la upendo mwaminifu ni lenye nguvu zaidi ya kifo na uhakika wa ufufuko.

Ee Bwana ufanye eneo hili lililobarikiwa kwa ajili ya marehemu waliokufa wakitetea uhuru na haki , tuvuliwe ule ubinafsi na sintofahamu na kwa njia ya upendo wako unaowaka,tusikilizea jina lako Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo, Mungu wa Yesu na Mungu aliye hai. Amina.

Na kabla ya Baba Mtakatifu Francisko kuacha makaburi hayo ya wayahudi huko Ardeatina, ameandika kwenye kitabu cha wageni maneno yafuatayo : "Haya ndiyo matunda ya vita, chuki, kifo na kulipiza visasi, utusamehe ee Bwana!

Sr Angela Rwezaula.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.