Yesu aliishi maisha yake yote akihubiri na kutenda kile ambacho kinahesabiwa na
muhimu yaani upendo. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyonena kwa nguvu kabla
ya sala ya Malaika wa Bwana kwa mahujaji wote waliokusanyika katika viwanja vya Mtakatifu
Petro Jumapili 29 Oktoba 2017. Baba Mtakatifu ameonesha kuwa, upendo unatoa msukumo
na kutoa maisha,ni safari ya imani kwa maana bila upendo maisha na imani vinabaki
tasa.
Akitakari Injili ya Siku kutoka (Mt 22,34-4), maahali ambapo Mwinjili Matayo anakumbusha
kuwa, wafarisayo wanatoa swali la mtego, juu ya amri ipi iliyo kubwa. Katika kuelezea,
Baba Mtakatifu anasimamia zaidi kufafanua juu ya upendo kati ya Mungu na binadamu.
Amekumbusha jibu lake Yesu:mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako
yote na akili yako na mpende jirani yako kama wewe binafsi.
Kwa njia hiyo Yesu anataka utambuzi ya kwamba bila upendo wa Mungu na jirani, hakuna
uaminifu wa kweli wa agano la Bwana. Baba Mtakatifu anaongeza, wewe unaweza kufanya
mambo mema mengi, hata kutimiza sheria, lakini kama hauna upendo mambo hayo hayasadii
kitu.
Akitaja kitabu cha somo la Kutoka, mara nyingine anasema, huwezi kuwa na agano na
Bwana wakati wewe unawatesa wale walio chini yako: hawa ni wajane, yatima, wageni,
wahamiaji yaani watu wote wapweke wasiokuwa na mlinzi. Baba Mtakatifu anasisitiza
kwa nguvu zote kuwa, sisi sote tumeumbwa kwa ajili ya kupenda na kupendwa kama Injili
inavyojieleza yenyewe ambayo inajibu shuhuku halisi ya moyo.
Mungu ni upendo anaendelea Baba Mtakatifu, ametuumba tuwe sehemu yake ya maisha, kwa
ajili ya kupendwa na Yeye na kwa ajili ya kumpenda, na ile kwa ajili yake tuwapende
wengine. Hiyo ndiyo ndoto ya Mungu kwa Binadamu. Ni ndoto inayowezekana kwa njia ya
neema yake tu, kwasababu sisi tunahitaji kuipokea ndani mwetu ili tuwe na uwezo wa
kupenda, upendo utokao kwa Mungu mwenyewe. Hiyo kwa dhati inatolewa na Yesu katika
Ekaristi Takatifu ambayo ipo kwa ajili ya kuelezea upendo wake mkubwa alio utoa yeye
binafsi kwa Baba yake kwa ajili ya ukombozi wetu.
Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, amewasalimia wahujaji wote walio kusanyika
katika uwanja wa Mtakatifu Petro ambapo Baba Mtakatifu amekumbuka kutangazwa kwa mwenye
heri mpya Giovanni Schiavo tarehe 28 Oktoba huko Caxias de Sul nchini Brazil. Alizaliwa
mwanzoni wa mwaka 1900 nchini Italia, lakini akatumwa kwenda kufanya umisionari akiwa
ni padre nchini Brazil na kujikita zaidi katika huduma ya watu wa Mungu na kwa kuwafundisha
watawa wa kike na kiume. Mfano wake, Baba Mtakatifu ameongeza, utusaidie kuishi kikamilifu
katika kumfuasa Kristo na Injili. Aidha amewasalimia wanajumuiya ya Togo wanao ishi
nchini Italia na wale wa nchi ya Venezuela, akiwakabidhi wote chini ya Mama Maria
wa matumaini hasa katika nchi zao.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |