2017-10-27 10:02:00

Papa ametembelea Jumuiya ya Taasisi ya Scholas Ocurentes Roma


Mchana wa tarehe 26 Oktoba 2017 Baba Mtaktifu amefanya matembezi yake mafupi kwa mara ya kwabza baada ya kuzundua shule hiyo mwezi Juni mwaka huu katika makao Taasisi ya Kipapa ya Scholas Occurrentes iliyoko katika Mtaa wa Mt, Calisto mjini Roma. Baba Mtakatifu amefika matendo ya Trastevere, mahali ambapo amepokelewa na wanafunzi wengi, pamoja na wakufunzi, walimu, wanafanyakazi, waandishi wa habari, watu kujitolea ambao wanajikita kuwasaidia vijana  na watu waliobaguliwa.

Scholas Occurrentes ni Taasisi ya Kipapa, iliyoundwa na Baba Mtakatifu tarehe 13 Agosti 2013 na tarehe 9 Juni 2017 ilizinduduliwa rasmi, yenye kuwa na  lengo la kuhamasisha na  kutetea, kwa njia ya elimu, sanaa na michezo, utamaduni wa kukutana kati ya vijana wa dini zote, ili kuchangia katika ujenzi wa jamii bora kupitia nguzo ya  mazungumzo  katika kuhakikisha amani duniani. Leo hii Scholas Occurrentes  imeshasimika mizizi katika nchi 190 duniani kote, ikiwa na  mtandao zaidi ya mashule 446,000 na mitandao ya kielimu  kwa madhehebu yote ya dini, umma na binafsi  ambapo Juni 2017 imekuwa na makao yake makuu katika mji wa wa Roma.

Ni fursa maalumu kwa Baba Mtakatifu kutembelea mji wa Roma kwa ajili ya Kipapa ambapo sasa naye anafanya sehemu ya shughuli za Scholasa , mahali ambapo anaweza kuwa na uwezekano wa kukutana na wanafunzi wanaosihi katika hali ngumu  kama alio kuwa amezoea wakati bado yuko katika nchi yake, kama vile Messico, Paraguay, Argentina, Portorico na Texas na kuwasikilia , lakini pia ushuhuda na msaada wa Scholas unaofanya kazi kwa ajili ya makataba wa shule kwa ngazi ya ulimwengu.

Baba Mtakatifu ameweza kuzungumza nao, lakini zaidi amesisitiza juu ya mada ya wahamiaji na mapokezi, iwe katika mabara vijana na yale mazee kwa mujibu wake anasema ni lazima kukabiliana na hali halisi na kusaidiana.Ametoa wito kwa watu wote kusiadia wahamiaji , maana wao ni ahadi ya wakati endelevu, lakini pia ameomba wahamiaji pia walinde watu wanao wapokea kwa kuheshimu sheria wanazokutana nazo.
Zaidi ya hayo amezindua madarasa 9 ya Scholasa kati yao ni kwa ajii ya nchi za Kati na Kusini mwa America.

Kwa sasa katika Taasisi ya Scholas, wapo hata vijana kutoka Palestina, Israeli, Uhipania na Italia.Roma kwa ajili ya wito, inayo nafasi ya uliwengu mzima kwa ajili ya mazungumzo na daraja la kuunganisha kati ya watu , amesisitiza maneno hayo Mwalimu Mkuu wa Taasisi ya Scholas Jose Maria del Corral. Hiyo ni Taasisi yenye vijana kutoka katika ulimwengu mzima kwa njia ya elimu iliyoanzishwa na Italia.

 Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.