2017-10-26 16:09:00

Papa:Utulivu wa roho ya mkristo unatokana na nguvu ya Roho Mtakatifu


Yesu anatualika kubadili maisha , kubadili njia na kutualika katika uongofu wa mioyo. Na hiyo inapelekea mapambao dhidi ya ubaya ambao umo ndani ya mioyo wetu, mapambano hayo hayaachi amani ndani ya mioyo. Ndiyo kiini cha  tafakari leo hii tarehe 26 Oktoba 2017 ya Baba Mtaktifu Francisko katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta Mjini Vatican. Mahubiri yake yametokana na Ijili ya leo kuhusu moto anaoutupa Yesu katika dunia. Baba Mtakatifu anasema, moto huo maana yake unatutaka tufanye mabadiliko.

Mabadiliko maana yake ni namna ya kufikiri nakubadili mtindo wa kusikiliza. Moyo wa  kiulimwangu, au upagani kikriso unageuzwa kwa nguvu za Yesu , kwa maana ya kubadilika ki ukweli na kuongoka. Mabadiliko ni namna ya matendo na  kwa njia hiyo ni katika matendo ambayo lazima kubadili.
Mabadiliko hayo siyo yale ya kujipakavipodozi usoni, bali ni madiliko ambayo yanafanywa na Roho Mtakatifu ndani ya Roho, anasema Baba Mtakatifu. Ni kujibisha katika njia ya roho mtakatifu maana yake ni kufanya mapambano ili kweli tendo hilo liweze kujitokeza ndani ya moyo na kuubadili.

Baba Mtakatifu anaongeza, hakuna mkristo yoyote ambaye ni mtulivu bila kuwa na mapambano ya kiroho. Kwasababu wale wasio kuwa wakristo ni vuguvugu . Anatoa mfano ya kwamba utulivu wa kulala unaweza kuupata kwa kumeza kidonge cha usingizi, lakini hakuna kidonge cha amani ndani ya roho, isipokuwa ni Roho Mtakatifu tu ambaye anaweza kukupatia utulivu wa roho na nguvu ya kikristo. Sisi lazima kusaidia Roho Mtakatifu anasema Baba Mtakatifu na kutoa nafasi yake ndani ya roho zetu.


Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.