2017-10-26 17:54:00

Papa: Utume wa kilei unajikita kwa mapana katika kiroho,familia na kijamii


Ninawasalimia ninyi nyote manudhuria wiki ya 48 ya kijamii kwa Wakatoliki nchini Italia,huko Cagliari.Salma kwa nama ya pekee Kardinali Gualtiro Basseti , Mwenyekii wa Baraza la Maaskofu wa Italia Askofu Mkuu Fulippo Santoro, maaskofu wote waliopo, na wajumbe wote kamatati ya kisayansi, na watayarishaji, aidha wawakilishi wote kutoka majimbo yote ya Italia, vyama vya kitume na mashirika mengi yanayojihusiha na kazi na wageni.
Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko kwa njia ya video kwa wajumbe wote wa Mkutano wa Wiki ya 48 ya kijamii kwa wakatoliki nchini Italia ambao umeanza huko Cagliari tarehe 26- na utamalizika 29 Oktoba 2017.

Baba Mtakatifu Francisko anasema kuwa wao wanaunganika chini ya ulinzi na mfano wa Mwenye heri Giuseppe Toniolo, ambaye mwaka 1907 alianzisha Wiki ya kijamii nchini Italiwa. Ushuhuda wake wa kilei , umejikita katika mapana ya maisha, ka mfano kiroho, familia, kitaaluma, kijamii na kisiasa. Ktika kazi yao , baba Mtakatifu anawashauri kujikita kwa undani mafundisho yake, kama vile alvyoandika: ni kugeuka kwa kina ndani ya moyo yule anayejikita kwa undani zaidi kulinda jamii iliyoyp na siyo tu katika diplomasia , au kusifiwa au shujaa , bali kuwa mtakatifu na jamii ya watakatifu”.

Baba Mtakatifu anasema, kwa maneno hayo, basi fanyeni tunu ya kumbkumbu msingi amabayo inatakatifuza katika kufanya kazi kwa ajili ya wengine , na kuongeza historia hiii ya tendo la uumbaji wa Mungu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.