2017-10-21 15:26:00

Papa:Jiepushe na ubishi wa kidunia, wengine wamejidai wakapoteza Imani


Ninakutana na ninyi katika tukio la miaka 300 ya hupatikanaji wa sanamu ya Mama yetu wa Aparecida. Shukrani kwa Kardinali Sergio da Rocha kwa maneno ya hotuba yake kwa niaba ya Jumuiya wanabrazili wa Taasisi ya Kipapa ya Pio hapa Roma, vilevile watawa wote wanaoshikiriana pamoja ili kuwezesha uwepo wa sehemu ndogo ya Brazil mjini Roma. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, asubuhi ya Jumamosi tarehe 21 Oktoba 2017 alipokutana na wanachuo wanajumuiya kutoka Brazili wanaosoma Roma wa Taasisi ya Kipapa kuungana na Baba Mtakatifu kama sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya miaka 300 ya upatikanaji wa sanamu ya Mama Maria, sikukuu iliyofanyika nchini Brazili hivi karibuni na ni sikukuu ya taifa lao.

Baba Mtakatifu anabainisha jinsi gani ya kujisikia vema katika mazingira ya ukarimu hasa, inapotokea unakuwa mbali na nchi yako au kujisikia ukiwa! Sehemu ya ukarimu inasaidia kushinda matatizo na kukubali hali halisi ambayo  shughuli za kichungaji siyo tena kiini cha siku. Anabanisha kuwaeleza kuwa wao sasa siyo maparoko au wasaidizi wa parokia, bali ni mapadre wanafunzi. Hali hiyo inaweza kupelekea hata ukosefu wa msimamao kati ya misingi inaysosimia maisha ya kikuhani. Baba Mtakatifu anabainisha misngi hiyo minne kuwa ni ukubwa wa kiroho, ukubwa wa masomo, ulkubwa wa kibanadamu na mwisho kichungaji. 

Kwa namna ya pekee katika kipindi cha maisha yao hasa kwenye sehemu ya mafunzo ndiyo yanachukua nafasi kubwa, lakini pamoja na hayo, haina ya maana ya kutojikita hata katika sehemu nyinginezo.Ni lazima kuwa makini katika kutunza maisha ya kiroho na hiyo ni katika misa za kila siku, sala za kila siku masifu, tafakari, na makutano binafsi na Bwana na kusali Rosari. Jambo muhimu pia kwa kwa mujibu wa uwezekano amewashauri kuwa ni vema kufanya hata shughuli za kichungaji.

Kwa upande wa ukubwa wa kibinadamu, Baba Ntakatifu anasema, inahitaji zaidi kuhepuka hali halisi ya utupu utokanao na upweke,kwasababu nyakati za kipindi chao cha masomo hakuna kitulizo kutoka kwa watu wa Mungu walio kuwa wamewazoea kwenye shughuli za kichungaji na hivyo muda wao wote wanamalizika katika utume wa masomo. Kudharua ukubwa huo , Baba Mtakatifu anabainisha kuwa ndipo milango mingine inafungua magonjwa , ambayo yanaweza kuwaambukiza mapadre wanafunzi, kama vile kusoma tu na vishawishi vya kufanya masomo ikawa ndiyo msingi binafsi. Kesi hizo mbili anaonya kuwa uhishia kukandamiza imani, badala ya kwamna ni  utume wa kutunza kama ambavyo  Mt. Paulo alimwambia  Timoteo kuwa  tunza salama yote  uliyokabidhiwa. Jiepushe na majadiliano ya kidunia na ubishi wa kipumbavu juu ya kile wanachokiita wengine “Elimu”. Maana wengine wamejidai kuwa na hiyo elimu na matokeo yake wamepoteza imani (1 Tm 6,20-21).  Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa wasisahau kwamba kabla ya kuwa walimu na wanasheria wao ni lazima kubaki mapadre na wachungaji wa watu wa Mungu!

Kwa njia hiyo anapata wazo tena kuwa anafikiria  kwanini Paulo aligusia juu ya masengenyo hayo : kwa manana masengenyo ndiyo yanayo haribu udugu wa kikuhani. Masengenyo ni tendo la ugaidii kwa maana anayesengenya anasema, ni kama  anarusha bomu na kumwaribu mtu mwingine alafu anaondoka kwa utulivu, Baba Mtakatifu anahimiza watunze undugu wa kikuhani . Aidha anatoa  mfano kuwa ingekuwa vema kuweka tangazo katika lift,au katika ubao wa matangazo mahali pa makaribisho, lisemalo hapa hakuna masengenyo badala yake, kuna Ukimya wa Maria , “Hakuna masengenyo “  ni ujumbe wa Vatican lakini hata unawahusu kwa maana nao  wanatenda hayo  anaosema Baba Mtakatifu.

Je hiyo inawezekanaje kubaki na msimamo sawa  kati ya misingi hiyo minne ya maisha ya kikuhani? Baba Mtakatifu anatoa jibu kwamba, ili kuhepuka na hatari hiyo ni lazima kufanya undugu wa kikuhani. Kwa maana msingi mkuu wa mafunzo ya kikuhani unakabiliana na mada ya mafunzo ya kudumu ambayo inasisitiza sehemu ya kwanza ya kukuza ya mafunzo ya kudumu ni ile ya undugu wa kikuhani (Ratio Fundamentalis  n 82).

Na hiyo ndiyo msingi ya mafunzo ya kudumu anasema, kwa maana   inasimamia wakati wa kutoa daraja takatifu la upadre, wate ni kushiriki umoja wa kikuhani na Kristo na kuunda familia moja. Neema ya sakramenti hiyo inakuza mahusiano ya kibinadamu na kisaikolojia, kujionesha kwa dhati katika aina nyingi za pamoja, siyo tu za kiroho bali hata zile za kimwili ( Jonh Paul II Pastores dabo vobis 74)

Baba Mtakatifu anafafanua kwamba  jambo msingi la kutambua wajibu wao wa upendo wa kichungaji  ni ule wa kufanya undugu kikuhani kama asemavyo Mtakatifu Paulo kwa Wagalatia "chukulianeni mizigo yenu na hivyo mtatimiza sheria ya Kristo". (Gal 6,2). Baba Mtakatifu anawapa ushauri kwamba wasali  pamoja kwa kushirikina furaha na changamoto za maisha ya mafunzo , kuwasaidiwa wale ambao wanajisikia upweke, watoke nje kwa pamoja kufanya matembezi, na kuishi kama familia ya ndugu bila kumwacha mtu yoyote pembeni na kutambua matatizo ambayo yanaweza kujitokeza kwasababu undugu wa kikuhani haumwachi mtu nyuma.

Aidha anasema watu wa Mungu wa Brazil wanawapenda na wanataka kuona mapadre wanapendana na kuishi kindugu, kwa namna hiyo pia  amewakumbusha changamoto za nchi ya Brazili inayowasubiri. Katika hilo anaongeza kuwakumbusha kipindi kigumu cha kihistoria ambacho nchi ya Brazili inaishi , mahali ambapo watu wanaonekana kukosa matumaini ya siku sijazo kutokana na matatizo ya kijamii na kafsha za ufisadi. Nchi ya Brazil inahitaji mapadre wake wawe ishara ya matumaini, anasisitiza Baba Mtakatifu na kuongeza kusema kuwa inataka kuona mapadre wanaungana kwa pamoja katika mapambano dhidi ya vizingiti, bila kutumbukia  katika vishwaishi vya uongozi au kushika nafasi. 

Na mwisho amewataka mapadre wanafunzi kuimba daima wimbo wa Mama wa Mbinguni ambaye nchini Brazil wanamwita Mama wa Aparecida kwa wimbo wa («Virgem santa, Virgem bela; Mãe amável, mãe querida; Amparai-nos, socorrei-nos; Ó Senhora Aparecida»). 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.