Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumapili tarehe 15 Oktoba 2017 kwa ajili ya kuwatangaza watakatifu wapya waliotetea imani yao hadi kufikia mauti, amewashukuru waamini na watu kutoka mataifa mbali mbali waliokuwapo katika Ibada Kuu ya kuwatangaza Watakatifu wapya. Kwa namna ya pekee, amewakumbuka wawakilishi maalum kutoka nchini Brazil, Ufaransa, Italia , Mexco, Kisiwa cha Malta na Uhispania. Baba Mtakatifu anasema, kwa maombezi ya mashahidi wa mwanga wa Injili , waweze kutusindikiza katika safari na kusaida kuhamasisha daima mahusiano ya kindugu, mshikamano kwa ajili ya Kanisa na jamii.
Aidha anasema, katika kupokea maombi ya baadhi ya Mabaraza ya Maaskofu wa Amerika ya Kusini pia sauti mbalimba kutoka kwa wachungaji na waamini kutoka baadhi ya pande za dunia, ameamua kuitisha Sinodi maalum ya maaskofu wa Makanisa za Panamazon, Sinodi itakayo fanyika Roma mwezi Oktoba 2019. Lengo msingi wa kuitisha Sinodi hii, Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, ni kuweza kuchanganua njia mpya za uinjilishaji kwa zile za watu wa Mungu wa asili, ambao daima wamesahaulika na kukosa msimamo wa sasa na nyakati endelevu na utulivu. Baba Mtakatifu anaongeza, hiyo inatokana na kipeo cha msitu wa Amazon ambacho ni kiini cha mtaji muhimu katika sayari yetu. Kwa njia ya Watakatifu wapya wasaidie maombi kwa ajili ya tukio hilo la Kanisa ili kwa heshima ya uzuri wa uumbaji, watu wote duniani wamsifu Mungu Bwana wa ulimwengu na katika mwanga wake waweze kutembea kupitia njia za haki na amani.
Vile vile Baba Mtakatifu amekumbusha kuwa, Jumanne tarehe 17 Oktoba 2017 ni Siku ya Kupamba na Umaskini Duniani. Baba Mtakatifu anasema, umaskini siyo maafa nazo sababu zake ambazo ni lazima kutambuliwa na kuondolewa ili kuheshimu hadhi ya ndugu kaka na dada wengi kwa mfano wa hawa watakatifu.
Sr angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |