2017-10-15 15:27:00

Misa ya Watakatifu wapya 35:Bila upendo maisha ya mkristo ni tasa


Saa 10 Asubuhi ya siku ya Jumapili tarehe 15 Oktoba 2017, katika Viwanja vya Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Francisko ameadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya kuwatangaza watakatifu wapya wa Kanisa 35 ambao ni Andrea de Soveral, Ambrogio Francesco Ferro, padre wa Jimbo , Matteo Moreira, mlei na wenzake 27 wafia dini; vijana wafiadini Cristoforo, Antonio na  Giovanni; Faustino Míguez, Padre Msikolopi na mwanzilishi wa Shirika la kitawa la Wakalasanziani wa Mabinti wa mchungaji; Angelo wa  Acri ambaye ni Padre wa Shirika la ndugu wadogo Wafranciskani hawa ni Baba Mtakatifu Francisko alikubali maombi ya kutangazwa kwao tarehe 20 Aprili 2017.

Baba Mtakatifu katika mahubiri amechambua Injili ya siku ya Jumapili inayozungumza  juu ya Ufalme wa Mungu kama sikukuu ya arusi (Rej: Mt 22,1-14). Anasema, aliye mstari wa mbele ni mtoto wa mfalme na Bwana arusi ambapo ni rahisi kumfikiria  kuwa ni Yesu. Lakini katika  maelezo hayo hawasemi juu ya  bibi arusi, bali wote wamealikwa , wanatamaniwa na kusubiriwa na ndiyo hao watakao vaa nguo ya arusii. Baba Mtakatifu anaongeza, wote walioalikwa ni sisi wote kwasababu Bwana anataka kufanya sherehe ya arusi na kila mmoja wetu.

Arusi inamaanisha  muungano wa maisha yote, ndiyo shahuku ya Mungu kwa kila mmoja. Kwa njia hiyo mahusiano yetu na Yeye hayawezi kuishia katika kufuata mfalme tu bila sababu msingi, au kama  watumishi na bwana wao tu au wakuu wa mashule na walimu wao. Hawali ya yote Baba Mtakatifu anasema ni kuona kuwa ni bibi arusi mpendwa na Bwana arusi. Kwa maana nyingine, Bwana anatamani, anatafuta, na kualika, kwa maana hafurahishwi au kutosheka na jinsi tunavyowajibika katika sheria basi. Yeye anatataka umoja wa kweli na thabiti katika maisha, anataka uhusiano wetu uwe wa mazungumzo, imani na msamaha wa kweli.

Baba Mtakatifu Franciko anasisitiza, hayo ndiyo maisha ya kikristo, historia ya upendo na Mungu, mahali ambapo Bwana kwa utashi wake amezisha upendo huo wa bure kwa kila mmoja, sisi tnaweza kufaidika tu katika kupokea huo mwaliko, kwa maana hakuna anayefaidika zaidi ya mwingine, kwani kila mmoja anayo fursa ya kufaidika mbele ya Mungu. Kwa upendo wa bure, wa ukarimu na fursa, ndipo kunatokea maisha daima ya kikristo. Baba Mtakatifu anatoa mfano: inawezekana kuuomba angalau mara moja kwa siku, kukiri kwa Bwana upendo wetu kwake Yeye, na iwapo tutakumbuka kati ya maneno mengi kwa siku  mwambie “Bwana ninakupenda na wewe ndiye maisha yangu”.Baba Mtakatifu anafafanua zaidi, iwapo upendo huo unapotea, maisha ya mkristo yanakuwa tasa na kuwa na mwili bila roho na kuwa na maadili yasiyowezekana ambayo ni pamoja na msingi na sheria ambazo zinaongoza bila ya kuuliza kwanini. Baba Mtakatifu kwa njia hiyo anasisitiza ni zaidi, Mungu wa maisha anasubiri jibu la maisha, Bwana wa Maisha anasubiri jibu la upendo.

Katika kitabu cha Ufunuo Bwana anakemea Kanisa lake kuwa, “lakini ninalo jambo moja dhidi yako : wewe hunipendi tena sasa kama pale awali” (Uf 2,4). Baba Mtakatifu anaonesha kuwa ndiyo hatari hasa ya maisha ya mkristo katika shughuli za kila siku, mahali ambapo anafurahia ukawaida bila ile kuwa na  kasi, au hakuna shauku,wala  kuwa kumbukumbu ndogo. Kwa njia hiyo anashuri kuiishi kumbukumbu ya upendo wa kwanza, kwa sababu sisi ni wapendwa, tumealikwa katika arusi na maisha yetu ni zawadi kwasababu kila siku  ni maajabu na fursa ya kuitikia mwaliko huo.

Injili ya leo inataadhalisha jambo fulani ya kwamba unaweza kukataa mwaliko. Kwa maana wengi walialikwa wakasema hapana , kwa maana hawakujali na wakaenda katika shamba na biashara zao kama isemavyo Injili ya Mtakatifu Matayo(Mt 22,5). Pamoja na hayo kuna neno “binafsi” ndiyo ufunguo wa kutambua sababu ya kukataa kwao.

Waaalikwa hawakuwa wanafikiria kama arusi ingekuwa ya uchungu au furaha, bali wahakujali , walikuwa wameshilia mambo yao, ndiyo alikuwa zaidi badala ya kujiweka katika mchezo kama upendo unavyotaka. Baba Mtakatifu anatoa mfano, hiyo ndiyo sababu msingi ya kwenda mbali na upendo, siyo katika roho mbaye, bali ile ya kupendelea mambo binafsi, uhakika, kujotosheleza, kujiamini  na hali nzuri binafsi.

Kwa njia hiyo ndiyo maana watu wa namna hiyo upendelea kukalia juu ya viti vya faida, raha na mazoe mengine ambayo hufanya ufurahi kidogo, lakini hayo yanafanya kuzeeka haraka na vibaya, kwasababu ni kuzeeka ndani ya moyo, maana  moyo huo haupanuki bali kujifunga. Baba Mtakatifu anafafanua zaidi kuwa, na hasa kila kitu kikitegemea umimi, kile ninachohitaji, kile nisichokihitaji, au kuwa mgumu na ukatili, na tabia mbaya kama ya wale waalikwa wa Injili waliofikia hatua ya kutoa maneno mabaya hadi kuwaua wale waliopeleka mwaliko kwa maana walikerwa.

Injili ya leo inauliza ni upande gani wa kukaa? katika upande wa umimi au wa Mungu: Lakini kwa utambuzi ya kwamba Mungu ni kinyume na ubinafsi na kujitosheleza. Pamoja na hayo Injili ya leo inatoa mwito wa kutokusimama  bali kwenda mbele japokuwa wapo wanaokataa mwaliko huo, ni kuendlea na sikukuu npia kuwendelea kutoa mwaliko kwa wengine bila kuchoka. Mungu hakati tamaa hata kwa wale wanaofunga milango yao, hata mbele ya ukosefu wa haki  mana anatoa jibu kwa upendo mkubwa.

Baba Mtakatifu anaendelea kusema tumezoa sisi tunapoonewa na kuwa na majeraha au kukataliwa, daima ni kutunza hasira. Hiyo ni tofauti na Mungu mwenyewe mbele ya watesi wake, na  hapana  zetu za kila siku, Yeye hachoki kutoa wito  na kualika kwenda mbele kuwaandaalia hata wale waliotufanyia mabaya. Ni upendo unaofanya hivyo kwasababu ya kushinda ubaya, anasema Baba Mtakatifu. Leo hii Mungu hasiyepoteza matumaini, anatualika kufanya kama yeye, kuishi kwa mujibu wa upendo wa kweli kwa maana unazidi hali ya kukata taama na vurugu zetu au uvivu.

Lipo  jambo moja la mwisho ambalo Injili inasisitiza: nguo ya wageni ambayo ni muhimu. Baba Mtakatifu anasema haitoshi kujibu mara moja mwaliko na kusema  "ndiyo" inatosha, lakini pia  unahitaji kuvaa nguo. Kwa maana halisi inahitajika kuwa na tabia ya kuishi upendo kila siku. Kwa maana ”si kila aniambiaye Bwana Bwana ataingia katika ufalme wa mbingu ila ni yule tu anayetimiza mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” (Rej Mt 7,21).
Kuna ulazima wa kuvaa nguo ya arusi kila siku ya upendo wake na kurudia kwa upya kufanya uchaguzi wa Mungu. Watakatifu waliotangazwa leo hii ni wafia dini ambao zaidi wanalekeza njia hiyo. Wao hawakusahau ile  ndiyo ya upendo kwa maneno  muda mfupi waliitikia ndiyo  katika maisha yao yote hadi mwisho. Nguo yao ya kila siku ilikuwa ni upendo wa Yesu ambaye alitupenda hadi mwishona kuacha msamaha wake na nguo zake kwa wale waliomsulibisha.

Hivyo na sisi tuliopokea nguo nyeupe wakati wa ubatizo ni nguo ya arusi na Mungu. Tumwombe kwa njia ya maombezi ya  ndugu zetu hawa watakatifu waliochagua kuvaa kila siku nguo ya arusi na kubaki nayo ikiwa safi. 
Je nifanye je? .  Baba Mtakatifu anajibu, ni kwa njia ya  kupokea msamaha wake bila kuogopa, ndiyo hatua ya dhati ya kuweza kuingia katika ukumbi wa arusi ili kuadhimisha sikuu ya upendo na Yeye.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.