2017-10-14 15:41:00

Papa anasema Mfalme Carlo ni mfano wa kuigwa kama Baba wa Familia


Katika ukumbi wa Clementina mjini Vatican, Jumamosi asubuhi ya tarehe  Baba Mtakatifu Francisko , amekutana na kuzungumza na wanachama wa sala wa Mwenyeheri Mfalme Carlo kwa ajili ya amani kati ya watu wa nchi na  duniani. Anamshukuru Mwenyekiti Askofu Mkuu mstaafu Fernand Frank wa jimbo Kuu la  Luxembourg kwa ajili ya hotuba yake. Mkutano wao wa Mwaka katika mazingira ya Roma unajikita katika muktadha wa miaka 100 ya kuwanzishwa kwa sala ya amani chini ya usimamizi wa Papa Benedikto XVna  kati ya wahusika wa kisiasa walio muunga mkono ni Mfalme Carlo katika shahuku ya kuona uwepo wa mwisho wa Vita ya Kwanza ya Dunia.

Kati ya malengo ya mshikamno wa sala, Mwenyekiti amesisitiza kuwa, ni kutafuta na kutunza mapenzi ya Mungu, kwa kuwajibika katika kukuza amani, haki na  katika kuendeleza kwa waasisi wa historia walionzisha , kwa namna ya pekee  katika maisha ya mwenye heri Carlo, ambaye alikuwa ni mwanaume na baba wa familia na pia kama mtoto wa Kanisa.
Yeye katika kujikabidhi katika mapenzi ya Mungu alikubali mateso na kutoa maisha yake kwa sadaka kwa ajili ya amani, akiongozwa ndaima na upendo na imani kwa mke wake Mtumishi wa Mungu Zita.

Chamangamoto za nyakati zetu zinataka ushirikiano kwa watu wote wenye mapenzi mema , kwa namna ya pekee sala na sadaka. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anawaalika kubaki kidete  katika ahadi zao za kuwa washirika katika sala na shughuli binafsi  na hata katika jitihada za papa kwa ajili ya amani. Bila kujiegemeza katika sala ya waamini, Mfuasi wa Petro hawezi kutimiza wajibu wake wa kitume katika dunia, kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anaongeza kusema, “ ninategemea sala zenu”.

 Mfalme alizaliwa tarehe 17 Agosti 1897 huko Austria na mfalme Carlo ni sura msingi na matazamo wa historia ya Ulaya mpya. Yeye kama kiongozi Mkuu wa   nchi , alijiendeleza katika fadhila ya kikristo kwenye Vita ya Kwanza ya Dunia, kuwa mwangwi wa miito mingi ya Papa Benedikto XV aliyokuwa akitoa. Mfalme wa Austria, alionesha hata mfano bora na ushuhuda wa kuwa mchumba na baba wa familia. Alipofukuzwa na kupelekwa uhamishoni  katika kisiwa cha Madeira, kipindi cha mwisho wa maisha yake, alionja na kufanya uzoefu wa umaskini wa kukithiri na kukubali ugonjwa kama sadaka kwa ajili ya amani na umoja wa watu. Alikufa 1 Aprile 1922 uso wake ukiwa unatazama  Ekaristi Takatifu. Baba Mtaktifu nasisitiza kuwa na  huo ndiyo moto wa maisha yake : “wajibu wangu daima ni kujua zaidi na haraka na kufuata mapenzi ya Mungu kwa kwa dhati”.

Baba Mtakatifu anaeleza hisotia yake akiongeza kuwa, tarehe 3 Oktoba 2004 Mtakatifu Yohane Paulo II wakati wa mahubiri yake siku ya  kumtangaza Mwenyeheri, alisema Mfalme Carlo anatambua wazi wajibu wake katika huduma takatifu ya watu wake. Wasiwasi wake ulikuwa ni wa kufuatilia kikamilifu wito wa kikristo katika utakatifu na hata katika jitihada za kisiasa. Chama cha Mshikamano wa Sala cha Mfalme Carlo kwa ajili ya amani limetambuliwa tangu mwaka 1963 kama jumuiya ya sala.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.