2017-10-13 16:27:00

Ujumbe wa Papa Francisko kwa waathirika wa tukio la moto Brazil


Baba Mtakatifu Francisko , ametuma ujumbe wake, ukielekezwa kwa Askofu wa Janaùba, mons. Ricardo Guerrino Brussati nchini Brazil , ujumbe ulio tiwa saini na Kardinali Petro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, kufuatiwa na tukio moto uliounguza shule ya watoto wadogo sana. Katika ujumbe huo ambao umetangazwa moja kwa moja katika mtandao  Katoliki wa Majimbo nchini Brazil, Baba Mtakatifu, anasikitishwa sana na tukio hilo, anawatia moyo ndugu jamaa na marafiki wa waathirika wengi wa watoto katika moto uliounguza  shule hiyo. 

Moto huo unasadikika kusababisha karibia watoto kumi na wengine wengi kujeruhiwa kutokana na mlinzi wa shule hiyo. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anaonesha mshikamano na ukaribu katika huzuni wa familia nyingi wanao omboleza kwa ajili ya watoto wao na waathirika wengi sana. Hata hivyo anamwomba Bwana awape nguvu na hata walio jeruhiwa kupona haraka, awape ujasiri na kitulizo cha matumaini ya kikristo kwa wote walioathirika na janga  hilo la kutisha. Na mwisho natoa baraka zake za kitume.

Huo ni moto ulitokea katika shule ya watoto wadogo katika Jimbo la Janaùba Kaskazini ya Mkoa wa Minas Gerais nchini Brazil. Kwa mujibu wa vyombo vya habari mahalia, moto umesababishwa na Mlinzi wa shule aliyekuwa ameachishwa kazi  baada ya kuhudumia hapo kwa miaka 8 na alikuwa ana matatizo ya kiakili. Kwa njia hiyo tarehe 5 Oktoba baada ya mazungumzo na mkuu  shule ya watoto alijimimina  mafuta ya kulipuka juu yake na watoto pia jengo na kuwasha moto, kati ya waliojeruhiwa na moto wakubwa na watoto ni kama watu 40.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.