2017-10-13 16:44:00

Papa:Mchezo hauna mipaka katika ulimwengu, unaounganisha tamaduni zote


Ijumaa 13 Oktoba 2017, Baba Mtakatifu amekutana na kuzungumza na Wachezaji wa Olympics Maalum, wanaoshiriki mashindano ya Umoja wa Soka. Baba Mtakatifu anafurahi kuwapokea katika tukio la kuwania ushindani na  Jukwaa zima  lililoandaliwa na Olimpiki Maalum, anamshukuru  kwa namna ya pekee mwenyetiki kwa maneno yake hata vijana waliotoa ushuhuda wao. Anasema, wao ni ishara ya mchezo unaofungu macho na moyo katika thamani ya hadhi ya kila mtu  na  binadamu wote , la sivyo ingekuwa ni kitu cha kuhukumiwa na kubaguliwa. 

Baba Mtakatifu anaendelea na hotuba yake, kwa siku hizi wanatakuwa na fursa ya kutafakari juu ya umuhimu wa michezo wa umoja na wengine wasio kuwa na kasoro yoyote ya kimwili na  kiakilia kucheza pamoja. Hii ni hali halisi nzuri mnayojikita katika kupeleka mbele kwa juhudi na uhakika wa kuongeza matumaini chanya ya baadaye, yenye kuleta matunda katika michezo. Na ili kufanya, inakuwa kweli fursa ya pamoja isiyokuwa na ubaguzi. Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa, wasichoke kamwe katika ulimwengu wa michezo na kuwa na  wajibu wa kushirikiana ili kujenga jamii zaidi ya kindugu,  mahali ambapo watu wanaweza kukua na kuendelea ili kufikia mshikamano wa kweli na dhabiti. Kwa maana hiyo mchezo ni mojawapo ya lugha ya ulimwengu inayozidi tofauti za utamaduni, kijamii , kidini , mwili na hufanya kuunganisha watu,ili washriki mchezo mmoja, kuwa mstari wa mbele pamoja na ushindi au kushindwa pia.

Kanisa kwa upande wake, Baba Mtakatifu anathibitisha, linajikita kutia  moyo kwa kile kinacho anzishwa katika sekta  ya michezo, kuhamasisha wema wa watu na jumuiya. Hiyo ni dhahiri kwamba mchezo daima umeweza kuwasaidia watu wengi katika historia kwa namna fulani kutoka katika sehemu za pembezoni, umasikini,  majeraha au kuvunjika. Hadithi hizi zinatuonyesha jinsi ya kuchukua uamuzi na tabia ya wengine inavyoweza kuwa sababu ya msukumo wa kusudi na kuwatia moyo  na  faraja watu wengi katika nyanja zote za maisha yao.
 Baba Mtakatifu anawatakia kila  la kheri katika siku hizi ili waweze kuwa na furaha na utulivu. Kwa pamoja waweze kujenga na kuimarisha urafiki na mshikamano. Mwisho anawaomba sala kwa ajili yake na kuwabariki kwa baraka ya kitume na kwa familia zao .

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.