Ni Yesu Kristo peke yake atakaye tuokokoa na mashetani wanaotufanya polepole tuangukie katika malimwengu pia kutokoa hata kwa mambo ya aibu na ulaghai ambao Mtakatifu Paulo anautaja katika kitabu cha Wagalatia. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko asubuhi ya tarehe 13 Oktoba 2017 wakati wa mahubiri yake kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta .
Baba Mtakatifu akitafakari Injili ya siku kutoka kwa Mwinjili Luka, Yesu anasema iwapo ninamfukuza Belzeburi kwa mkono wa Mungu, kwa maana hiyo wakati wa ufalme wa Mungu umewafika. Baba Mtakatifu anatoa wito wa kufanya tafakari juu ya dhamiri hasa kujikita katika matendo ndiyo yatatufanya tuwe wa kweli na ili wajanja na walaghai wasije ingia katika maisha yetu ambao ni shetani.
Na Bwana anaomba kukesha ili kuhepuka kuingia vishawishi: kwa maana hiyo mkristo
daima anakesha, yuko makini kama walinzi. Injili inaelezea juu ya mapambano kati
ya shetani na Yesu, wakati wengine wanasema Yesu ana Belzeburi ili kuweza kufanya
hayo yote aliyokuwa anatenda .
Baba Mtakatifu anaenelea kusema, Yesu hasimulii historia tu, bali anasema ukweli:
roho mbaya inapotoka katika binadamu inakwenda na kuzunguka katika jangawa ikitafuta
mahali pa kutua, isipofanikiwa , inarudi mahali pale ilipotoka,mahali ambapo ilikuwa
inaishi kwa binadamu huru.
Kwa maana hiyo ndiyo uamuzi wa shetani kuleta marafiki zake wengine saba wabaya zaidi
yake, kwa njia ya kufanya hali ya binadamu huyo aweze kuharibika zaidi ya kwanza.
Baba Mtakatifu anaonya zaidi juu ya neno mbaya zaidi katika Injili kwamba ni kuonesha
nguvu ya shetani anapoingia kwa binadamu na mabavu zaidi.
Anafanya makazi ndani ya maisha ya binadamu, katika mawazo yake ma matarajio kwa
kumfanya afikirie anaishi vema na kumbe ameingiliwa katika moyo wake na kumbadilisha
taratibu bila kufanya vurugu kubwa. Shetani anapoingia taratibu katika maisha yetu
anabadilisha hata mantiki na kutupeleka katika malimwengu, na hiyo siyo rahisi zaidi
kutambuakwa maana anakuja kiujanja sana Papa anabainisha. Na ndiyo hivyo binadamu
aliyekombolewa , anaeuzwa na shetani na kua mkatili maana amejawa na malimwengu, hivyo
ndivyo anavyotaka kuingia katika ulimwengu. Baba Mtakatifu anaonesha njia za ulaghai
wa shetani maana anapoingia katika maisha yake kwa shangwe anatumia upole, anatawala
kila aina ya mtindo wa kuishi hata katika thamani zetu na juu kutoa huduma ya Mungu.
Mkristo anageuka kuwa wa malimwengu, anakuwa wa uvuguvugu, anakuwa na mchanganyo katika roho kidogo ya malimwengu, na roho kidogo ya Mungu, lakini yote hayo mi kinyume na matakwa ya Mungu.Baba Mtakatifu anajibu swali ya jinsi gani ya kufanya ili kuhepuka hatari ya hiyo kwamba, mada ya kuanguka katika vishawishi inawezekana kupingana bila kuogopa na kwa utulivu, ndiyo njia kubwa ya kuweza kuondokana na hira za shetani anayeingia taratibu katika maisha yetu.
Baba Mtakatitu anashauri njia za kufana kwamba, ni kukesha maana yake kutambua nini kinapita katika moyo, ni kutafakari na kufanya mang’amuzi ya maisha: nini maana ya kuwa mkristo?, ninajifunza au kuwafunza vema watoto? maisha yangu ni ya kikristo au ya malimwengu? Ninawezaje kutambua hilo? Na majibu yanatoka kwa Mtakatiff Paulo kuwa ni kutazama Kristo msulibiwa. Tunaweza kutambua hayo mahali ambapo msalaba wa yesu umefunjwa . Ndiyo lengo la Msalaba mbele yetu, msalaba siyo pambo tu.
Ni msalaba unatukoa na ira za shetani ambaye anatuongoza tutmbukie katika malimwengu.
Baba Mtakatifu anatualika kutazama Kristo msulibiwa, kwa maana tunapofanya njia ya
msalaba ni kutazama thamani kubwa ya wokovu na siyo tu kutazama dhambi bali hata
malimwengu.
Baba Mtakatifu anasisitiza kujitafuta dhamiri kuona ni kitu gani kinatokea katika
maisha . Lakini zaidi ni mbele ya Kristo Msulibiwa, Sala pia itakuwa vizuri inasindikizwa
na matendo ya upendo kwa ndugu,wagonjwa nakusaidia mtu aliye na shida. Hiyo ina maana
ya kwamba matendo ya dhati yanavunja uhusiano unaotaka kufanywa na mashetani saba
wanaotaka binadamu atumbukie katika malimwengu.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |