2017-10-12 15:53:00

Papa:Mara ngapi tumezoe kuuliza maswali kwanini mbele ya Mungu?


Tarehe 12 Oktoba 2017, saa 3 asubuhi, Baba Mtakatifu Francisko ametembelea Taasisi ya kipapa  kwa ajili nchi za ya Mashariki, baadaye saa 10: 15 ameadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya tukio la  miaka 100 ya  kundwa kwa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki  na Papa Benedikto wa XV kwa waraka  binafsi  wa Dei Providentis  tarehe 1 Mei 1917. 

Wakati wa mahubiri yake, Baba Mtakatifu anashuru Bwana kwa ajili ya kuanzisha Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mashariki na Taasisi za Mashariki , kwa njia ya Papa Benedikto  XV iliyotokea miaka mia moja iliyopita . Wakati huo ilikuwa ni vita vya  Kwanza vya dunia, leo hii pia inakumbusha kama ilivyokuwa wakati ule kwasababu tunaishi kwenye vita vingine vya dunia hata kama ni vipandevipande. Baba Mtakatifu anasema tunaona ndugu wengi wakristo wa Manisa ya mashariki wakifanya uzoefu wa mateso ya kutisha. Matukio hayo yanatoa maswali ya kujiuliza kwa nini.Maswali hayo yanafanana na yale yaliyojitokeza katika somo la  kwanza  kutoka  kitabua cha Malaki (3,13-20a).

Bwana analalamikia watu akisema: “Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema Bwana…. Lakini ninyi mwasema, tumesema nini dhidi yako, nyinyi   mmesema, kumtumikia Mungu hakuna faida; na tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za Bwana wa majeshi? Tuonavyo sisi ni kwamba, wenye kiburi ndiyo wenye furaha daima . Watu waovu licha ya kustawi, hata wanapomjaribu Mungu hawapatii adhabu”.

Baba Mtakatifu anatakari: ni mara ngapi hata sisi tunafanya uzoefu huo, mara ngapi tunasikia maneno hayo, hata katika maungamo ya watu wanaofungua mioyo yao wakisema: tunaona wabaya, wale wakatili , wasio jali wengine bali kwa maslahi yao, wanakandamiza wengine, utafikiri mambo yao yanakwenda vema wakiwa wamepata kile wanachotaka  wanafikiri kufurahia maisha ; Baba Mtakatifu anaongeza , ndiyo swali linakuja kwanini Bwana?
Habari  kuhusu  maswali ya kwanini yapo hata katika Maandiko Matakatifu ambayo hata binadamu wa leo anaendelea kuwa nayo.

Maswali hayo lakini  yanajibiwa na Neno la Mungu, hasa ni kutoka katika sehemu hiyo hiyo ya somo la Nabii Malaki: “ndipo watu wanaomcha mwenyezi Mungu walipomzunguka wao kwa wao,  naye Mwenyezi Mungu akasikia mazungumzo yao. Mbele yake kikawekwa kitabu ambamo iliandikwa kumbukumbu ya wale wanaomcha na kumheshimu” (Malaki 3, 16). Kwa njia hiyo Mungu hasahau watoto wake, kumbukumbu yake kwa wenye haki, wale wanaoteseka wakiomba kwa nini, na hawachoki  kumwamini Bwana.

Mara ngapi Mama Maria katika safari yake amenena akisema kwanini, lakini alikuwa akitafakari yote na kuyaweka ndani ya moyo wake, neema ya Mungu ilikuwa ikichanua imani na matumaini. Lakini ipo njia moja ya kufanya kumbukumbu ya mungu katika sala,  tunafundishwa na somo la Injili ya siku kutoka mwinjili Luka 11,5-13). Unaposali inahitaji ujasiri na  neema, kuamini kuwa Bwana anasikiliza, anatia moyo ili weza kubisha mlango. Bwana anasema kila aombaye  atapewa , atafutaye atapata na abishaye atafunguliwa, na kwa njia hiyo inahitaji ujasiri Baba Matakatifu anasisitiza.

Maswali ya Baba Mtakatifu: je sala zeti ni hakika kwa namna hiyo? Je sala hiyo inajikita kwa ndani ya moyo na katika maisha? Je upo utambuzo wa kubisha katika moyo wa Mungu?.  Mwisho wa Injili Yesu anasema mtoto gani akimwomba baba yake samaki  na akampa nyoka badala ya samaki  au kumuomba yai akampa lile la nge?. Kama ninyi ingawa ni waovu  mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi atawapa Roho Mtakatifu wale wanaomwomba.

Labda tulitegemea aseme kutoa jambo kitu chema machoni, lakini yeye anasema atawapatia Roho Mtakatifu wale wanao mwomba.  Na hiyo kwa dhati ndiyo zawadi kubwa zaidi ya Mungu Baba Mtakatifu ansisitiza. Zawadi tuliyopokea kutoka kwa Baba ni Roho; ndiyo zawadi ya kweli ya Baba wa mbinguni. Binadamu anabisha hodi mlango wa Mungu kwa njia ya sala ili kuomba neema. Yeye ni Baba  na  anatoa zawadi kubwa zaidi ya  Roho Mtakatifu . 
Amemaliza mahubiri yake akiwataka wote kijifunza kubisha hodi katika moyo wa Mungu, kujifunza hilo kwa ujasiri. Sala hii ya kijasiri na asili iweza kuchangia na kuimarisha hudumza zao katika Kanisa,  kwa njia ya jitihada hizo matunda yatakuwepo kwa wakati wake , hatimaye watakuwa kama miti yenye matawi yasiyo nyauka.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili  

 








All the contents on this site are copyrighted ©.