2017-10-10 15:45:00

Mungu ni mwenye huruma hata kwa wale wenye mioyo na vichwa vigumu


Katika siku mbili mfululizo, Liturujia inafanya tutafakari Kitabu cha Yona na juu ya huruma ya Mungu ambaye anafungua mioyo yetu na kushinda yote. Ni mhutasari unaokusanya mahubiri ya Baba Mtakatifu akichambua somo la kwanza, siku ya Jumanne 10 Oktoba 2017 katika Kanisa la Mtakatifu Marta Mjini Vatican. Hicho ni kichwa kigumu cha Nabii anayetaka kumfundisha Mungu namna ya kufanya mambo , pamoja na hayo sehemu ya mwisho itasikika kesho katika tukio ambalo kila mmoja analifahamu Baba Mtakatifu nasema.

Bwana anamuomba Yona aende katika Mji wa Ninawi kufanya utume  ili watu wapate kuongoka. Kwa mara ya kwanza Yona alitoroka na  kukataa kufanya hivyo, mara ya pili anakubali  na kufanikiwa, hata hivyo Baba Mtakatifu anaonesha kuwa, baadaye  nakuwa na hasira mbele ya msamaha anao utoa Bwana kwa watu waliomfungulia mioyo yao  kwa kutubu na kupata msamaha. Yona alikuwa na kichwa kigumu  na zaidi alikuwa ni mgumu wa moyo, mwenye ugonjwa wa ugumu na roho iliyogandamana.

Anafafanua na kusisitiza kuwa, kwa kawaida wenye kuwa na mioyo migumu , iliyo gandamana hawezi kujua huruma ya Mungu, kwa maana wao ni kama Yona anayefikiria kuwa hawa walipaswa kupewa hadhabu kwa ajili ya ubaya wao walio utenda na kwenda jehanamu. Wagumu wa mioyo hawajuhi kupanua mioyo yao kama alivyo Bwana. Wagumu wa mioyo ni waoga  kutokana na mioyo yao kufungwa na kufumbata sheria za haki. Hawa wanasahau kwamba haki ya Mungu imefanyika kwa njia ya mwili wa Mwanae mpendwa  , yeye ajifanya huruma, yeye ajifanya msamaha kwa maana  moyo wa Mungu daima ni wazi katika msamaha.

Wale ambao hujisahau na kuwa na vichwa vigumu, Baba Mtakatifu anaongeza,kwa dhati ndiyo ukuu wa Mungu unajionesha kwao  na zaidi kwa njia ya huruma na msamaha. Hata hivyo Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, siyo rahisi kutambua vema huruma ya Mungu, kwasababu inahitaji sala nyingi ili  kutambua neema hiyo msingi. Sisi tumezoea tabia  za kusema amenifanyia hili, naye atakiona!  Ambayo ni hali ya kulipiza kisasi, lakini Yesu mwenyewe  amelipa kwa ajili yetu na anaendelea kulipa hata leo hii.

Baba Mtakatifu anazidi kusistiza  juu ya historia ya Yona,  Mungu anarudi kila wakati, na kwasababu hiyo angeweza  kumwacha Yona aliyekuwa na kichwa kigumu na  ugumu wake , lakini alirudi kwake na kumfanya akubali  kumwokoa yeye binafsi hata watu wa mji wa Ninawi.  Kwa maana hiyo huyo ni Mungu mvumilivu, ni Mungu  anaye bembeleza na kupanua mioyo. Huo ndiyo ujumbe wa kitabu hicho cha kinabii , Baba Mtakatifu nathibitisha  kuwa ni mazungumzo kati ya unabii , kitubio , huruma na ugumu au kicha kigumu. Lakini pamoja na hayo, huruma ya Mungu inashinda daima maana ni mwenye nguvu inayojionesha katika huruma yake. 

Baba Mtakatifu anamalizia akiomba awashauri wote leo hii kuchukia Biblia na kusoma Kitabu cha Yona , kwa maana  ni kitabu kidogo chanye sura tatu tu. Katika kusoma watazame ,jinsi gani Bwana anatenda , ni jinsi gani ya huruma ya Mungu au ni jinsi  gani Bwana anabadili mioyo yetu , baada ya kuona hivyo, ni kumshukuru Bwana kwa maana ni mwingi wa huruma.

 Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya  Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.