Umoja ni zawadi ya Roho Mtakatifu, kwa njia hiyo, uekumene ni njia muhimu ambayo inatokana na sala kwa maana ni katika maombi ya pamoja, umoja huo unawezekana. Ni maneno yaliyo thibitishwa na Kardinali Kurt Koch Mwenyekiti wa Baraza ka Kipapa la Kuhamasisha umoja wa Kikristo, wakati wa kutoa hotuba yake katika Kanisa Kuu la Civitavecchia nchini Italia kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Kichungaji katika majimbo tarehe 6 Oktoba 2017.
Akichambua kwa undani zaidi juu ya umoja wa wawakristo, Kardinali Koch anatoa maelekezo ya historia ya mageuzi ya safari ya kiekumene, akianzia katika Hati ya pamoja ya Baba Mtakatifu Francisko na Askofu Younan Mwenyekiti wa Shirikisho la Makanisa ya kiluteri duniani uliotiwa sahini mwaka jana huko Sweden. Kwa upande huo Kardinali anasema, mchakato huo unaweza kufikia umoja, hasa kwa upande wa wakatoliki kuanza kuwa na upeo chanya na mpya juu ya mageuzi ya Kanisa la Kiinjili. Upeo huo ni kutoa tofauti zilizokuwapo katika hali ya wakristo wa mashariki ambao wamekabiliana nayo kwa miaka mini ya kale.
Kwa mujibu wa Kardinali, anasema hiyo inawezekana lakini , iwapo huruma na mapatano
yanazingatia na kufuta mwelekeo msingi wa safari ya kiekumene endelevu. Aidha anafafanua
kuwa pia inahitjai kuwa na mtazamo wa mafundisho kuanzia katika Maandiko ya Mtakatifu
na yale ya Mtakatifu Agostino mwaka 1530, hata mengine yaliyofuata yanayohusu
maungamo yake kwamba, muungano kamili wa kiekumene unawezekana kutokana na mabadiliko
ya kudumu ya Kanisa kwa njia ya Msingi Mkuu wa Injili na kutunza umoja wa Kanisa
ambalo linaungana bila kutenganishwa.
Kardinali ameweza pia ujibu baadhi ya maswali kuhusiana na suala hili , ambapo amebainisha
kuwa hakuna njia yoyote ya watu au mtaalamu wa mambo ya Mungu isipokuwa ni kwa njia
ya uekumene unaofanya wakristo wote katika hali zote. Kwa njia hiyo anatoa mwaliko
kwa kila mmoja kujenga,kuhamasisha, kuuliza na kujifuanza kutambua taalimungu ya Kanisa
lake, kwa kushirikiana kindugu na Makanisa mengine, lakini kuficha kuwa matatizo yapo
hasa yanayohusu mantiki ya mazungumzo ya pamoja.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |