Baba Mtakatifu ametuma barua iliyotiwa sahini na Kardinali Pietro Parolin Katibu
Mkuu wa Vatican kwenye Mkutano wenye kuhusu mada juu ya “Bahari yetu, ni bahari
kwa ajili ya maisha”. Ni mkutano wa siku mbili, tarehe 5 na Oktoba 2016 huko Malta.
Ujumbe huo umewakilishwa na Askofu Mkuu Silvano Tomas , ambaye ni mwanachama wa Baraza
la Kipapa kwa ajili ya Maendeleo ya Binadamu aliyeshiriki katika kazi ya mkutano
huo.
Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu, anatia moyo nguvu na jitihada za kukabiliana na
matatizo mengi ya haraka, kama vile biashara ya binadamu, utumwa, hali halisi zisizo
za kibinadamu katika kazi ndani ya viwanda vya uvuvi na biashara ya usafirishaji.
Aidha fursa za maendeleo ya jumuiya forodhani, familia za wavuvi na hali ya kutisha
katika visiwa vinaoshairiwa kukupotea kutokana na ongezeko la maji.
Bahari ni urithi wa pamoja katika familia ya binadamu, anaandika Baba Mtakatifu.
Haiwezakani kudharau hali ya kutunza urithi huo dhidi ya uchafuzi wa maji kwa njia
ya platiki nyingi ambazo matokeo yake ni mabaya ya afya na maisha ya binadamu anayefanya
kazi baharini.
Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu anachukua kipengele cha ujumbe wa Hati ya “Sifa kwa
Bwana” inayohusu ulinzi wa Mazingira nyumba yetu. Anasisitiza kuwa, haiwezekani
kuona wanapotea hata baadhi ya viumbe majini ambapo vinageuka kuwa makaburi ya viumbe
majini visivyo kuwa na rangi ya maisha.
Baba Mtakatifu anakumbusha jinsi asili ya kila kitu inavyohusiana na kwamba, bahari
zinaweza kuwa rasilimali msingi katika kupambana na umaskini na mabadiliko ya hali
ya hewa na kwamba, hayo ni matukio mawili ya karibu. Kwa njia hiyo anabainisha
kuwa hiyo ni kushindwa kwa mtu huyo anayetumia bahari kwa ajili ya uharibifu, akitupa
takataka na hutumiaji wa njia za kisasa za kumwaga uchafu wa tindikali utokanao na
uchimbaji madini chini ya baharini.
Baba Mtakatifu katika kipengele kingine cha ujumbe wa Sifa kwa Bwana anakumbusha umuhimu wa kuelimisha ushirikiano wa kibinadamu, mazingira ya pamoja, kuwafundisha vijana ili waweze kuwa makini katika hutoaji wa huduma bora, pia kuwasaidia kukua katika ujuzi na kutafakari juu ya ukuu na ukubwa wake. Anamalizia akisema kwa muda mrefu sana, tahadhari imezingatia hali ya uhalifu na maafa ya kibinadamu baharini, bila ujasiri wa kutosha kukabiliana na sababu zake, ambazo mara nyingi zinapatikana kwenye ardhi. Ni wakati sasa wa kufanya kazi na wajibu mkubwa zaidi kulinda bahari zetu, nyumba yetu ya kawaida, na ndugu na kaka na dada zetu, leo na siku zijazo.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |