Lugha mpya ni njia muhimu ya kutafakari ambayo haipunguzi katu lugha ambazo Kanisa kwa muda mrefu imekuwa ikitumia na ambayo inatoa fursa ya kuendeleza mazungumzo ambayo Bwana alitumia wakati ule kuelimisha watu ili waweze kujibu zawadi kubwa ya Mungu anayoitoa mwenyewe na kwa watu wote. Ni Maneno ya Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican, Monsinyo Dario Vigano akihutubia mapema wiki hii katika Toleo la 30 ya wiki ya Mafunzo ya Kitelojia yenye mada inayohusu lugha mpya za kuwasiliana huko Pistoia Italia.
Monsinyo Vigano katika hotuba yake, amejikita zaidi kuelezea lugha mpya na hasa
akitafakari juu ya mawasiliano ya Baba Mtakatifu katika Kanisa na kwa jamii. Njia
za kuwasiliana kwa Baba Mtakatifu katika Kanisa na jamii daima zinathibitisha hali
halisi ya tunavyoishi, kwa maana yeye anasisitiza umuhimu wa kusikiliza, kusikiliza
sauti za vyombo vya habari kwa makini, kuchambua mwelekeo wake na kuwa na subira katika
kutoa huduma kwa ajili ya Injili.
Tabia ya Baba Mtakatifu imejionesha hata wakati wa kutoa sauti za ukarimu na kuwasiliana,
ambayo Monsinyo Viganao anabainisha kuwa inakwenda kinyume na yule apigaye kelele
na kumfanya msikilizaji a hasiwe kufuata kwa makini kile kinachotolewa au kuzungumza.
Kwa njia hiyo, anatufundisha Baba jinsi gani ya kuwasiliana kwa ukarimu, upole , sauti
za chini na kusikiliza kwa makini.
Akitoa mfano halisi na rahisi ya mawasiliano ya Baba Mtakatifu anasema, Yeye
ana uwezo wa kuelewana na kila mmoja katika mitandao ya kijamii, kwa mfano kwa vijana,
kutumia selfie, kuwapigia simu watu wengi, na hiyo ndiyo tabia ya Baba Mtakatifu katika
mawasiliano yake.
Katika kuthibitisha zaidi anasisitiza akisema,Mawasiliano ya Baba Mtakatifu yanakwenda
sambamba na nyakati za sasa, mahali ambapo kuna hata mabadiliko ya mawasiliano Vatican.
Kwa mtazamo wa Mtakatifu Ignatio wa Loyola, anaendelea Vigano, Baba Mtakatifu ana
uwezo wa kumfikia kila mmoja, kujikita katika mawasiliano, siyo tu katika kusema na
kutenda, bali hata kusikiliza kwa makini na kutambua jinsi gani ya kuweza kusaidia
inapobidi kwa hali halisi. Hiyo ndiyo kutambua kwa macho na moyo wa upendo wa Mungu.
Uhusiano wa Baba Mtakatifu ni ule unaojikita katika jadi anasisitiza, kwa maana ya mazungumzo ya moja kwa moja na vijana, kwa wale wote wenye kuwa na sababu, kama vile wenye imani haba au wasio jihusisha kamwe na imani. Aidha anasema, Baba Mtakatifu anayo karama na zawadi ya ukaribu na jirani, hiyo imeweza kujionesha na kushuhudiwa wazi na wengi katika matendo yake ya kila siku, ni katika maneno na mifano mingi inayojieleza kwenye maisha yake ya kawaida ya kila siku.
Monsinyo Vigano anabainisha pia juu ya muhimu na mtindo wake wa kuwasiliana,
kama vile kuinamia watu, kuwapokea, ucheshi, hizo ni mifano rahisi lakini, pamoja
na ishara mbalimbali rahisi za kila siku katika kutumia lugha rahisi ya moja kwa moja,
hata kile kitendo cha kubeba mkoba wake bila kusaidiwa na mwingine, ndiyo njia ya
lugha mawasiliano ya Baba Mtakatifu.
Mwisho Monsinyo Vigano anasisitiza juu ya ulazima wa mwamini kuishi kama anayefanya
mazoezi ya shahuku ya mambo ya Mungu. Ni kwa njia hiyo tu sote tutakuwa ni jumuiya
iliyofanikiwa yaani ni Kanisa ambalo linajihusisha kuwasilisha kwa furaha Injili
na uwepo wa Injili hiyo katikati ya watu bila ya ubaguzi.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |