2017-10-05 15:48:00

Papa:Tafuta mizizi yako ya asili,siyo kujitosheleza na uhamisho kisaikolojia


Anayepata mizizi yake ni mtu mwenye furaha, wakati uhamisho wa kujitosheleza binafsi wa kisaikolijia humfanya mtu vibaya sana, kutokana na kwamba huondoa mizizi ya asili. Ni maneno ya tafakari la Baba Mtakatifu Francisko asubuhi ya Alhamisi 5 Oktoba katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta akitafakari katika somo la kwanza kutoka kitabu cha Neemia.

Katika kitabu hicho kinaeleza umati mkubwa wa kiliturujia kwamba,ni watu walikusanyika katika mlango wa maji huko Yerusalemu. Na ndiyo ulikuwa mwsho wa hisotoria ya uhamisho wa Babeli, ambao ulidumu kwa miaka 70. Hiyo ni historia ya machozi ya watu wa Mungu.  Baada ya kuanguka kwa ufalme wa Babeli kwenye mikono ya Waajemi, Mfalme wa Kiajemi aliomwona Nehemia, akiwa na huzuni wakati anamimina divai kwenye kikombe chake, akaanza kuzungumza naye. Neemia alionyesha hamu yake ya kutaka kurudi Yerusalemu maana alikuwa anali ana kukumbuka nchi yake.

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu pia anafakari zaburi ya Zaburi 137. Isemayo “Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni.   Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu.3 Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni. Tuuimbeje wimbo wa Bwana Katika nchi ya ugeni? Ee Yerusalemu, nikikusahau wewe, Mkono wangu wa kuume na usahau. Ulimi wangu na ugandamane Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka. Nisipoikuza Yerusalemu Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu.”

Katika Zaburi hiyo, Baba Mtaktifu anafikiria hamu na shahuku ya wahamiaji ambao wanatoka mbali na nchi zao, wanataka kurudi makwao. Anakumbuka pia ishara iliyofanyika mara baada ya misa katika ziara yake ya kitume huko Genova. Kwamba, walimalizia wakitumbuiza wimbo unao wahusu  wahamiaji waliokuwa wanahamu ya kuwa katika maeneo hayo lakini, walikuwa mbali. Baba Mtakatifu anaendelea na tafakari kuwa, Neemia anandaa safari ya kurudi na ili kuwapeleka watu wake huko Yerusalemu. Hiyo ni safari ngumu Baba Mtakatifu anabainisha, kwa maana ilimtaka atafute njia ya kuwafanya wakubali  mawazo yake ya , kupeleka vitu kwa ajili ya kuujenga mji , nguzo , ekalu, lakini cha zaidi ilikuwa ni safari ya kwenda kutafuta mizizi ya watu. Baada ya miaka mingi mizizi ilianza kuwa dhaifu lakini haikupotea. Kwa njia hiyo kuitafuta mizizi maana yake ni kufanya sehemu ya watu wako, anasema Baba Mtakatifu. Bila mzizi siyo rahisi kuishi na ndiyo maana watu bila mizizi au kuachana na mizizi hiyo, maana yake ni watu wagonjwa anathibitisha. Aidha anafafanua kuwa, mtu anayesahau mizizi yake binafsi ni mgonjwa. Kugundua mizizi binafsi, na kuipa nguvu yake ili iweze kutoa matunda ni kama asemavyo mshahiri kwamba : nguvu ya kutoa maua katika mti inatokana na nguvu iliyoko kwenye mzizi ardhini, ndiyo maana ya  uhusiano kati ya mzizi na mema ambayo hatuwezi kufanya.

Lakini katika safari hiyo, Baba Mtakatifu anabainisha vizingiziti vinavyoweza kuwapo  kwamba, haiwezekani pasiwepo matatizo. Hiyo ina maana kwamba kushindwa ni kwa wale ambao wanapendelea kukaa uhamisho, maana ya kwamba, iwapo hakuna uhamisho kimwili, kuna uhamisho wa kisaikolojia kwa mantiki ya uhamisho binafsi wa jumuiya, na  kijami kwa wale ambao wanapendelea kuishi bila mzizi. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anasema,tunapaswa kufikiri juu ya ugonjwa huu wa uhamisho kisaikolojia, ambao hutufanya kutbaki na mizizi na kuondoa ushiriki wetu.Hufanya mtu vibaya kwasababu huondoa mizizi na kutoa ushiriki wetu.

Hata hivyo watu walikwenda mbele na kifika siku moja katika ujenzi wa mji. Watu hao walikusanyika pamoja ili kurejesha mzizi yao, Baba Mtakatifu anathibitisha, walisikiliza Neno la Mungu ambalo Mwandishi Ezra alisoma. Na ndipo ikatokea kilio, japokuwa wakati huu haikuwa kilio cha Babeli, ilikuwa ni kilio cha furaha, kukutana na mizizi yao, kukutana na mali yao mwenyewe. Na  Baada ya kusoma, Neemia anawaalika wafanye sikukuu.  Mtakatifu anathibitisha, hiyo  ni  furaha kwa wale ambao wamepata mizizi yao.

Kwa maana hiyo, mtu anayepata mizizi ya asili yake, ambao ni uaminifu wa Mwanamume na mwanamke ambaye hupata mizizi yake mwenyewe, wanawakilisha wale  waaminifu katika kufanya sehemu ya ushiriki wao.  Ni mwanamume na mwanamke mwenye furaha na furaha hiyo ndiyo nguvu zao. Baba Mtakatifu anaongeza, hiyo ina maana ya kutoka katika kilio cha huzuni kutokana na umbali na mizizi yao, na watu wake, kugeuka kuwa machozi ya furaha kwa maana wamefika nyumbani na kuwa sehemu ya watu wa nchi pamoja kutoka ugenini, maana ni nyumbani  kwao.

Baba Mtakatifu amewaalika  kusoma kwa makini sura ya nane ya kitabu cha Neemia , na katika kusoma, watafakari kwa kina wakikumbuka Bwana. Aidha kama wameanza safari ya kutafuta mizizi yao ya asili, au wanapendelea kukaa uamisho wa kisaikolojia ambayo ni njia ya ubinafsi . Anawataka pia wasiwe na hofu ya kulia kwa maana, baada ya kulia kwa huzuni baadaye watalia kwa furaha. Ni lazima kuomba neema ya kulia kwa kwa uchungu juu ya dhambi zetu , kuwa na huzuni kwa ajili ya dhambi zetu, lakini kulia pia kwa furaha kwa sababu Bwana amesamehe dhambi kama alivyo fanya kwa watu wale . Na mwisho kuomba neema ya kujiweka katika safari ya kutafuta na kukutana  na mzizi binafsi ya asili ya maisha yetu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.