2017-10-02 14:43:00

Papa Francisko aunda Jimbo Jipya la Francistown, Botswana!


Baba Mtakatifu Francisko ameanzisha Jimbo Jipya la Francistown, lililoko nchini Botswana na kuliweka kuwa ni sehemu ya Jimbo kuu la Pretoria, Afrika ya Kusini. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Monsinyo Franklyn Atese Nubuasah, S.D.V, kuwa Askofu wake wa kwanza. Jimbo jipya litakuwa na Parokia 17 zinazohudumiwa na Mapadre 26 wakisaidiwa na watawa 28 kutoka katika Mashirika sita ya kitawa yanayofanya kazi Jimboni humo! Kwa bahati nzuri, pia kuna mtawa wa kiume katika Jimbo hili jipya!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.