Kila tarehe 29 Septemba Kanisa Katoliki linafanya sikukuu Malaika watatu walinzi nambao ni Mikaeli, Gabrieli na Raffaeli. Malaika Gabrieli ni msimamizi wa Radio Vatican, ambapo misa takatifu imeadhishwa katika Kanisa la Mtakatifu Maria wa Traspontina mjini Vatican. Katika misa hiyo Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican ameadihmisha misa hiyo akiwa na mapadre wengine wa Radio Vatican.Kwenye mahubiri yake anasema tunakutana pamoja katika altare kwa ajili ya kuadhimisha sikukuu ya msimamiz wa Radio Vatican Gabrieli pamoja na wenzake Michaeli na Rafaeli, mahali ambapo Kanisa limewaweka pamoja katika kufanya sikukuu ya wajumbe wa Mungu.
Uwepo wa mwanga katika roho za watakatifu hawa Malaika inatusindikiza katika kusikiliza
neno na kuumega mkate wa maisha. Monsinyo Vigano anauliza, Malaika ni nani?. Katika
kujibu swali hili anasema, kulingana na Maandishi ya Matakatifu na mapokeo ya kanisa
inatoa mitazamo miwili kuhusu malaika hawa. Kwa upande mwingine Malaika ni kiumbe
hai mbele ya Mungu ambaye yupo mbele ya Mungu na mahali popote, kwa maana ya kwamba
katika majina matatu ya malaika yanaishia na elufi ya EL maana yake
ni Mungu, Mungu ameandikwa katika majina yao maana ni asili yao. Asili yao ya kuishi
ni uwepo kwa ajili ya yake na tabia ya Malaika ni wajumbe wa Mungu. Wao wanapeleka
ujumbe wa Mungu kwa watu. Kutoka kwa Mungu wanakaribia watu katika ardhi, wao hurudi
kwa Mungu, kwa maana wao wanaisha daima na Mungu wakati huo huo wako karibu na binadamu.
Malaika wanaalikwa kutusindikiza sisi wenyewe, na kufanya uzoefu wa ukarimu na upendo
wa mungu ambaye anatukaribisha na kutukumbatia ili tuweze kuondona na udhaifu wa kila
aina. Kwa njia hiyo anasema Monsinyo Vigano tunagundua wito wetu kuwa na sisi tunageuka
kuwa malaika kwa wengine, Malaika daima anaongoza katika njia njema na kuepusha
njia pofu
Hiyo ni wazi anasema kwasababu mapambano ni hali halisi ya kila siku kama ilivyoeleza
somo la kwanza. Kwa maana aliye na shahuku ya kufuata Bwana lazima ipo kazi kubwa
katika moyo katika maisha familia, kazini , watu , katika jumiua zetu za Kanisa.
Lakini Bwana ameweka karibu hivi viumbe vyenye mwanga ili giza la migogoro visiwe
n anafasi ya kutishia na uzito wa mapambano usishinde furaha yetu. Wimbo wa mwisho
katika kitabu cha ufunuo , unasema, Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni
ikisema: “Sasa umefika ukombozi na nguvu na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo
wake! Maana yule aliyewashtaki ndugu zetu mbele ya Mungu ametupwa chini. Naam, ametupwa
chini huyo anayewashtaki usiku na mchana.(Ap 12,10).
Kitabu cha ufunuo ni cha aina yake kwa mana ni tukio linalijikita kila siku katika
maisha yetu na hasa inapotokea kipindi cha kupambana kati ya mema na mabaya , mwanga
na giza. Ni juhudi ambayo leo hii tunaalikwa kuchagua mema ambaye ni Kristo. Aliye
tumia vema uhuru wake, na kupokea kwa huruma na msamaha wa baba yake kwa njia ya
damu ya mwanae akatufanya hata sisi tuwe watoto wa Mungu.
Hatuna haja ya kuogopa anasema Vigano, kwasababu ubaya hautakuwa na neno la Mwisho. Injili inahakiki kwamba Yesu ndiye anayetupeleka kwa Baba ,kwa kupitia katika ngazi ya msalaba wake , na zaidi ndiye yeye aliyesulibiwa. Kwa njia ya Yesu msulibiwa Mungu anajionesha katika ardhi na kupaa mbinguni , Yeye ndiye daraja pekee kati ya mungu na binadamu. Yote yanatokea kwa njia ya mwili wake na nyama yake iliyosubiliwa ili nasi tupate maisha.Katika matukio yetu, shughuli zetu na matatizo yetu Mosninyo Vigano anasisitiza, tumwachie yeye katika mwanga wa kweli na Mungu.Yeye Kamwe hatuachi pekeyetu na kusamehe pia.Hata sisi kama Malaika Gabrieli tunaweza kutangaza habari njema. Yeye alipeleka habari kwake Maria ya kwamba atakuwa mama wa Mtoto wa Mungu, alipeleka habari kwa Zakaria juu ya kuapzaliwa kwa Yohane.
Katika kazi yetu, tunaalikwa kusambaza habari njema ya ya maisha , uzuri, mshikamano na kushirikisha. Monsinyo Vigano ametoa onyo kuwa, inabidi kutambua kile ambcho tunatamka. La sivyo ni hatari kwamba tunapiga kelele ambayo haiwezi kuzaa matunda ya kusikiliza kwa dhati na hasa katika kusikiliza ziel habari za kweli za mawasiliano. Hata sisi tunaalikwa kuwa malaika walio tayari kama Kristo ili kuweza kuishi ndani ya binadamu. Tunaalikwa kujitoa kushinda kila siku ya na kujiweka tayari katika ngazi zote zinazopelekea kukutana na Bwana , katika hali halisi ndogo ya kila siku. Ametoa mfano kuwa, Mwanamme kila siku anapanda ngazi kwa ajili ya mke wake, mama anatelemka ili aweze kupokea mwanae, aidha mgonjwa anakabiliana na ugonjwa wake. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko anatoa wito ,malaika ni roho wa utume , waliotumwa kuhudumia wale ambao ni warithi wokovu.Hivyo ni lazima kuwa na utambuzi wa uwepo wao japokuwa hawaonekani. Tuombe kila wakati kwa kukumbuka uwepo wa Mungu, watusindikize katika mapambano dhindi ya mabaya na kutufikisha katika njia ya hakika ya maisha yetu.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |