2017-09-29 16:53:00

Kard. Parolin:Mpango Marshall kwa ajili ya Wakristo nchini Iraq


Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican ametoa hotuba yake tarehe 28 Septemba 2017 katika Mkutano kuhusu mpango wa Ujenzi wa mji na Vijiji vya  Wakristo wa Bonde la Ninawi. Kardinali anashukuru Shirika la Kipapa kwa ajili ya Kanisa hitaji kwa ajili ya kuandaa Mkutano huo na kushiriki kwake. Aidha amewasalimia baadhi ya washiriki wa Mkunao huo, kwa namna ya pekee Louis Raphael I Sako, Patriarki wa  Babilonia na Wakaldayo, Yohanna Petros Mouche, Akofu Mkuu wa Mosul, na Nicodemus Daoud Matti Sharaf, Askofu Mkuu wa Kiorthodox  wa Mosul. Anawashukuru wote kwa ukarimu wao katika Kanisa ambalo linakabiliana na  matatizo hasa ya wakaristo wa Bonde la Ninawi ikiwa ndiyo lengo kuu la Mkutano huo.

Kardinali Parolin anasema, Baba Mtakatifu amefuatilia kwa wasiwasi mkubwa tangu mwanzo wa kipeo cha maelfu ya familia ambao wamelazimika kukimbia miji na vijiji vyao kutokana na kuingiliwa na Serikali ya Kiislam tangu mwaka 2014. Anakumbusha kuwa, baada ya miezi miwili Baba Mtakatifu alikuwa amemwandikia barua  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  wakati ule Ban Ki Moon,  akiomba jumuiya ya kimataifa kusaidia wakristo na makundi mengine yaliyokimbia kutokana na ukatili wa kigaidi ili waweze kurudi katika vijiji vyao kwa usalama . ( Barua ya Baba Mtakatifu kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Agosti 2014).

Wasiwasi huo umeendelea  pamoja na kwamba  matendo ya kidiplomasia ya Vatican, yameonesha mekuwa mstari wa mbele, kuingilia kati kwa kutoa  misaada  wakizingatia mahitaji hasa yale makuu ya  watukuweza kurudi katika maeneo yao lakini  zaidi  kuhakikisha juu ya usalama, ulinzi na haki zao. Katika mikutano mingi kwa ngazi ya kimataifa, Vatican haikosi  kuonesha kuwa ,uwepo wa wakristo ni msingi katika nchi za Mashariki yenye  amani, thabiti na  muungano wa tamaduni na kutoa mchango mkubwa kwa karne nyingi.

Uwepo wao pia unazidi kuleta wasiwasi  mkubwa kutokana na wimbi kubwa la kuhama kwa familia nyingi kutoka katika maeneo ya kihisotoria, mahali amabapo wamekaa kwa muda wote wakitafuta usalama na maisha bora endelevu. Katika Hati ya Kitume kwa Makanisa ya Mashariki, Baba Mtakatifu mstaafu  Benedikto XVI  anakumbusha kuwa, nchi za mashari bila au kuwa na wakristo wachache , siyo tena Mashariki , kwasababu tangu kale wakristo wameshirikishana na waamini wa madhehebu mengine ule uzalendo wa kale katika kanda hizo.

Kwa maana hiyo,  Kardinali Parolini, anaongeza, wote tunao utambuzi ya kwamba migogoro na mivutano ya miaka ya hivi karibuni , inahatarisha namna ya kuishi kwa  wakaristo kuishi mahalia ambapo kuna uzushi wa makundi ya kuleta utofauti. Kutokana na suala hilo  Vatican inasisitiza daima umuhimu wa utetezi wa kuendelea kuwapo wakristo kwa njia ya zana za kisheria , haki za binadamu wakimbizi katika maeneo yao na kuhakikiaha kuwa hali ya usalama, heshima ya uhuru wa dini na zaidi, umuhimu wa uwezekani wa mantiki ya usawa kwa hali zote na uwajibikaji. Zaidi lazima kukabiliana na matukio ya kigaidi na sababu zake , kwa njia ya mazungumzo ya kidini, kutambuana na elimu.

Pamoja na  changamoto zilizopo lazima   kuunda hali ya kijamii kisiasa na kiuchumi  ili kufanya muungano wa pamoja katika kuhamasisha maridhiano, amani kwa ajili ya wakristo na baadhi ya madhehebu madogo na uwezekano wa ujenzi wa nchi endelevu na  misingi ya madhubuti. Wakristo wanahitjai kutambuliwa uzalendo wao na kuwa na ulinzi kama wazalendo  wa nchi za mashariki. Kwa njia hiyo mchakato wa ujenzi mpya ulioanzishwa na  mashirika haya ili kuwafanya wakristo waweze kurudi katika maisha yao ya kawaida ni wazo nyeti, la kipaumbele katika juhudi hizo. Jitihada hizi zitawafanya jumuia ya  kikristo kukabiliana na changanmoto nyingine lakini wakiwa mikononi mwa watu wenye ukarimu na mapenzi mema ya ujenzi wa jumuiya ya amani katika nchi nzima.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.