2017-09-28 16:46:00

Papa: tusiogope kutubu dhambi zetu kwa dhati maana dhamiri inauma


Tusiogope kusema ukweli juu ya maisha yetu kwa kuzingatia dhambi na kukiri kwa Bwana ili aweze  kutoa msamaha. Ni ushauri wa Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa mahubiri yake tarehe  28 Septemba 2017 katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican akitafakari Injili ya Siku. Injili ya siku ilikuwa inaelezea hofu ya Erode  aliposikia mahubiri ya Kristo. Baba Mtakatifu anakumbusha jinsi wafuasi wengi walivyo mfikiria Yesu kabla ya kutambua yeye ni nani hasa, maana wengine walifikiri kuwa ni Yohane mbatizaji, Elia au nabii. Na Erode hakuwa anajua ni nani  kwa njia hiyo angeweza kufikiria nini?. Alikuwa na wasiwasi katika moyo wake, na ndiyo maana alitafuta njia ya kumwona Yesu ili aweze kutulia. Alitaka kuona miujiza aliyoitenda Yesu lakini hakuweza kuitenda mbele yake, na ndiyo maana alimkabidhi kwa Pilato na Yesu akalipa kwa mauti.

 Baba Mtakatifu nathibitisha kwa njia hiyo alijifunika uhalifu juu ya mtu mwingine, lakini alisumbuliwa na  na dhamiri pamoja na uhalifu mwingine , kama vile kuua kwa hofu. Baba Mtakatifu anaongeza,kusumbuliwa na dhamiri siyo jambo rahisi la kukumbuka  tu juu ya kitu, lakini ni kidonda ndugu cha hatari ndani ya moyo. Hilo ni donda kubwa na la kuhumiza  iwapo katika maisha tumewahi kufanya jambo baya . Lakini ni kidonda  cha siri ambacho huwezi kuona kwa macho, hata mtu mwenyew binafsi  kwa maana amezoea kubeba hilo donda  la moyo kwa siri na baadaye anageuka kama kapigwa sindano ya usingizi. Baba Mtakatifu anasema, wapo wengine wanaogusa, lakini kidonda hicho kipo ndani . Na iwapo sasa kidonda kinaumiza, ni kuhisi vurugu za ndani na dhiki kubwa  katika mwili, katika dhamiri binafsi hadi katika maisha yote. Na hapo ndiyo kuna kishawishi cha kufunika ili usiweze kusikia tena.

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anasema inahitajika neema ya kutubu kwa Mungu  dhamiri hiyo  kwa maana kuna jambo,lakini pia  Baba Mtaktifu anasema,  hakuna aliye mtakatifu ingawa wote mara nyingi tunatazama dhambi za wengine na siyo za kwetu , wakati huo inawezekana wengine wanateseka kwa ajili ya vita au udikiteta unao sababisha hata kuuwa watu. Kwa namna hiyo ni mwaliko wa Baba Mtakatifu  kutoa jina la kidonda ndungu cha roho , je hilo donda ndugu liko wapi ?. Anatoa ushauri ya kwamba hawali ya yote inabidi kusali  ukisema Bwana nihurumie mimi mdhambi. Bwana anasilikiliza sala zako, pia tafakari dhamiri ya maisha yako, na iwapo huoni ule uchungu unatoka wapi wakati ni dalili yake, ni lazima kuomba msaada kutoka kwa mtu mwingine uli uweze kutoa nje hilo donda la roho lialogusa dhamiri.

Iwapo dhamiri yako ina aibu , ni kwa sababu umefanya hivyo kwa hakika, na huo ndiyo unyenyekevu wa kweli mbele ya Mungu na Mungu anasikiliza mbele ya mtu anayetubu kwa dhati dhambi zake. Baba Mtakatifu aidha anelezea ukweli wa dhati unaojieleza kwa watoto wadogo wanapofanya kitubio. Ni udhati wa kusema kweli kile ambacho kimetendeka, ili kuweza kutoa ukweli nje na kupona ndani ya nafsi yako.
Ni vema kujifunza sayansi na  hekima ya kujihukumu wewe binafsi. Unapojisikia dhamiri yako na uchungu wa kidonda ndugu, lazima kufanya kila iwezekanalo kutambua ni wapi limetokea, baada ya kujua dalili zake, jihumu binafsi. Usiwe na hofu ya kushitaki dhamiri , maana ni dalili za wokovu. Jamo la kuwa na  Baba Mtakatifu anasema ni kufunika, kupaka rangi juu na  kuficha, hiyo ndiyo hofu kwa maana inahitajika uwazi kwa Bwana ili aweze kukuponya. Anamalizia akiomba neema Kwa Bwana ili aweze kutufanya wajasiri wa kujihumu sisi wenyewe ili tupate kutembea katika njia ya msamaha.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.