2017-09-28 17:04:00

Kardinali L. Sandri anafanya Ziara yake katika nchi ya Romania


Kuanzia usiku wa tarehe 27 Septemba  hadi Jumapili 1Oktoba Kardinali Leonardi Sandri  Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili Makanisa ya Mashariki anafanya ziara katika nchi ya Romania. Ziara yake imendaliwa na Mwakilishi wa Vatican nchini humo  na mwaliko kutoka kwa Kardinali Lician Mureşan, askofu Mkuu wa di Făgăraş na Alba Iulia ya Romania katika tukio kuadhimisha miaka mia moja ya Baraza la Makanisa la Mashariki.
Ratiba ya ziara yake inatazamia kutembelea majimbo ya kilatini ya Lasi kuanzia 28 Septemba  akikutana na ma hali  halisi ya matendo ya upendo  na kubariki makanisa, na  altare mpya katika Kanisa makanisa mahalia.

Tarehe 29 atakuwa Bucarest mji mkuu wa Romania mahali ambapo ratiba inaonesha kukutana na  Patriaki wa Kiorthodox Daniel , mshauri wa Rais wa Jamhuri ya nchi hiyo  Bw. Sergiu Nistor na baadhi ya Mabalozi , zaidi atabariki Jimbo la Mtakatifu Basilio Mkuu iliyojengwa mwaka 2014, pia  Kanisa moja karibu na Kanisa Kuu la Kilatini la Mt. Yoseph.

Jumamosi 30 atatembelea Blaj , mji Mkuu wa kitasaufi ya Kanisa la Kigiriki katoliki  huko Romania, na makao makuu ya Askofu  Mkuu. Atakutana na Kiongozi Mureşan, na Sinodi ya Maaskofu  wa Kigiriki Katolini. Vile vile atatembelea Kambi ya uhuru, mahali ambapo wameweka ishara  kwa ajili ya tukio la Miaka 100 ya Baraza la Mashariki na Mahusiano ya Kanisa la Kigiriki Katoliki huko Romania.

Tarehe 1 Oktoba ; Kardinali Sandri anatarajiwa kuadhimisha misa takatifu akiwa pamoja na Kardinali Mureşan kwenye Kanisa Kuu la kiaskofu.  Baada ya misa anatarajiwa kubariki Kanisa jipya katika mtaa mmoja wa kabila la Waromania.  Kardinali Sandri atawafikisha kwa wote makuhani, waamini viongozi wa nchi salam za  upendo kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko. Baba Mtakatifu anawatumia baraka zake kwa ajili ya shughuli na ukarimu wa matumaini kwa Bwana na zaidi, Baba Mtakatifu anawatakia safari njema ya mazungumzo ya kiekumene. Jioni ya Jumapili tarehe 1  anatarajiwa kurudi Roma.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.