2017-09-25 15:52:00

Mahubiri ya Papa kwa Vikosi vya Ulinzi Vatican, Jumapili 24 Sept 2017


Katika somo la kwanza Nabii Isaya anatoa ushauri wa kumtafuta Mungu na kuongoka: mtafuteni na yeye anapatikana. Baba Mtakatifu ameanza na maneno ya somo kutoka katika kitabu cha  Nabii Isaya katika mahubiri yake kwenye Grotto ya Vatican kwa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Vatican, Jumapili 24 Septemba 2017.

Baba Mtakatifu anasema, upo uongofu, kwasababu ni njia ile ambayo nabii anasema tafuteni Bwana kwa maana anapatikana. Kubadili Maisha na kuongoka, ndiyo njia ya kweli. Pamoja na hayo Yesu mwenyewe anabadili mantiki  zaidi ya ile ambayo  kila mmoja hasingeweza kutambua, hiyo ndiyo mantiki ya upendo wa Mungu. Anatoa mfano kwamba, wakati mwingine ndiyo wewe utafanya kila njia ya kutafuta Bwana, lakini la muhimu utambue kuwa ni yeye aliye wa kwaza kukutafuta. Aidha wakati wa kutafuta Bwana ni muhimu kutambua kuwa ni yeye wa kwanza anayekutafuta.

Akitafakari kuhusu Injili ya siku anasema, ni Mungu anayetoka kutafuta watu wake. Katika Injili inaonesha kuwa ni mara tano, Mungu anatoka katika sura ya  mkuu wa nyumba anayekwenda kutafuta wafanyakazi kwenye shamba lake. Baba Mtakatifu anaongeza, siku maana yake ni maisha ya mtu, kwa maana  Mungu anatoka ndani ya nyumba asubuhi, katikati ya asubuhi, saa sita, alasiri na jioni saa 11 . Ni Baba asiyechoka kutoka nje . Ni Mungu mwenyewe ambaye hachoki kutafuta watu wake wote wawe na utambuzi ya kwamba Mungu anatupenda.

Baba Mtakatifu anaendelea na tafakari, ni mara ngapi watu wengi wanashinda viwanjani  na mitaani kama wale watu waliotajwa kwenye Injili  kwa siku wakiwa peke yao, katika dunia, na wakati mwingine ni wadhambi. Wakiitwa njiani rudi  hawataki bali ni kusema tumechelewa. Lakini kwa upande wa Mungu hakuna kuchelewa, hiyo ndiyo mantiki ya uongofu. Yeye mwenyewe anatoka nje kutafuta, kwa maana hiyo alianza kutoka yeye mwenyewe kwa kumtuma mwanae wa pekee akatafuta wale waliopotea. Mungu wetu daima anaendelea kutazama wanae.

Mfano mwingine Baba Mtakatifu anasema, fikirieni mtoto mpotevu: baba yake alimwonaje  kwa mbali? Ni kwasababu kila siku labda alitoka nje  akitazama kama angetokeza mwanae kurudi nyumbani. Huo ndiyo moyo wa Mungu wetu anayetusubiri daima Baba Mtakatifu anathibitisha. Na iwapo mmoja anaweza kusema amempata Mungu, anakosea kwa maana ni Mungu aliyemtafuta  akiwa wa kwanza. Ni mungu anayefanya hatua ya kwanza , kwa maana ya kwamba yeye hachoki kamwe kutoka nje, anasubiri daima uhuru wa kila binadamu, anasubiri binadamu afungue mlango wake kidogo. Hilo ndilo jambo kubwa mihimu la Bwana ambaye ni mnyenyekevu. Ni Mungu mnyenyekevu anayesubiri binadamu muda wote .

Kwa njia hiyo binadamu wote wadhambi wanahitaji kukutana na Bwana,  ili kupata nguvu za kuendelea mbele zaidi, kuwa wema na rahisi. Jambo hilo lakini linahitaji kuwa makini, wasababu Mungu mwenyewe anatafuta kila siku, Baba Mtakatifu anasisitiza. Ni jambo baya sana kuona Mungu anapita  lakini bila kumtambua. Leo hii ni kuomba neema ya kuweza kutambua, wakati huo huo kuwa na uhakika kwamba yeye anasubiri pamoja kwamba tu wadhambi, wadhaifu na matatizo, lakini haijalishi yeye anazidi kusubiri.

Baba Mtakatifu Francisko amemalizia mahubiri yake akiwataka wote waombe kuwa na neema hiyo ya kutambua Bwana  anapopita, pia ufahamu ya kwamba Mungu daima anasubiri kila mmoja lakini pia wasiwe na hofu kwasababu, hata mtoto mpotevu alipokutana na baba yake,  baba yake alitelemka mbio kumlaki mwanae, aliyetamka kuwa amekosa mbele yake na Mungu pia.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.