2017-09-22 12:55:00

Ask. Mkuu Ivan Jurkovič: Jamii za watu asili zitambuliwe haki na heshima yao


Kuheshimu haki na tamaduni za watu wa asili, ndiyo wito mkuu uliotolewa tarehe 20 Septemba 2017 na Askofu Mkuu Ivan Jurkovič, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican kwenye ofisi za  Umoja wa Mataifa huko Geneva, katika kikao cha 36  cha Baraza la  Haki za Binadamu kwa namna ya pekee kuhusu mada ya  “watu asili”. 

Katika hotuba yake, Askofu Mkuu Jurkovič, anasisitiza kuwa  wote lazima wawe watenda wakuu kwa ajili ya hatima yao. Mandeleo kamili yakibinadamu na mazoezi kamili ya heshima ya kibinadamu hayawezi kubatilishwa kwa njia yoyote, lakini  kila mtu, kila familia lazima iwe na fursa za kujiendeleza. Dhana ya ubora wa maisha, haiwezi kufanyika kutoka nje, anaendelea Askofu Mkuu,  akitaja maneno ya Papa Francisko kuwa, ni lazima kukubaliana na desturi ya kila kikundi cha binadamu. Na ndiyo maana ulinzi na uendelezaji wa maisha ya kiutamaduni, kijamii na kiuchumi ya watu wa kiasili unaweza hutambuliwa na wote kama huduma inayofanywa kwa familia ya wanadamu  hata kwa vizazi endelevu.

Kwa mantiki ya watu wa asili, Askofu Mkuu ameonesha kuwa, Vatican inajikita kikamilifu katika kuendeleza  na kutafuta ushirikiano na watu wa kiasili kwa mfano katika kuandaa vitabu vya sarufi na tafsiri katika lugha zao  ambazo mara nyingi inashiria kupotea lugha hizo, pia kutoa masaada katika kulinda haki zao za utamaduni, kijamii, kisiasa na kuchumi. Pamoja na hayo Askofu  Mkuu amekazia juu ya kukuza ulinzi na ushirikiano wa Jumuiya za watu  asili ndani ya dhana ya kitaifa na kimataifa na kueleza kuwa, heshima ya kutambuliwa kwa tamaduni na mazoezi ya jadi za asili huchangia maendeleo ya mazingira katika mazeozi endelevu na usimamizi sahihi wa mazingira yenyewe. Jamii za asili  anasema Askofu Mkuu  Jurkovič, siyo ya watu wachache kati ya wengine, lakini pia wao lazima wawe  watendaji na washiriki  wakuu wa mazungumzo inapotokea mapendekezo ya mipango mikubwa inayohusu ardhi zao za asili. 

Kwa mantiki hii Askofu Mkuu anabainisha kwamba, Vatican imekuwa mara nyini inasisitiza kuwa tatizo la mahusiano ya mazingira  kati ya makampuni ya Kimataifa na watu asili, hasa katika maeneo ya viwanda vya madini, lazima kukabiliana nayo; na kwa njia hiyo, mazungumzo yawe ya kweli na wazi. Ni lazima kukubaliana kati ya sehemu zote mbili zinazohusika ili mwisho wake watu wa asili  waweze kukubali kwa uhuru kwa lengo la maendeleo muhimu na kamili ya binadamu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.