2017-09-20 14:52:00

Vijana 100 huko Madaba kwa ajili ya Kambi ya Amani ya Vijana duniani


Ni karibia vijana 100 kutoka ulimwenguni ambao wamefika Madaba nchini Jordan ngome ya Wakristo wa Mashariki. Vijana hao ni kutoka katika nchi ya Italia, Uhispania, Argentina, Ureno Ethiopia na Lebano wanaoudhuria Kambi ya amani ya Vijana duniani, ilioandaliwa kwa ushirikiano wa Chama cha Vicentina, Caritas ya Jordan, Living Peace. Tangu tarehe 17 hadi 22 Septemba vijana hao watajikita katika shughuli za kujitolea kwenye makambi ya wakimbizi kutoka nchi za Siria na Iraq walioko katika nchi hiyo ya Jordan.

Kati yao kuna hata vijana 30 wakristo kutoka katika miji ya Aleppo ambao kwa msaada wa Caritas wameweza kupata visa ili kuweza kushiriki nao katika tukio hilo. Ni uzoefu wa aina yake ambao unawasilisha ujumbe wa amani na ukaribu kwa watu wa nchi ya Jordan. Anayasema hayo Giovanni Zambo mmoja kati ya waanzilishi wa “Chama cha kupinga  Vita” akiwa moja kwa moja katika kambi ya parokia cha Roho Mtakatifu  Hinina huko Jordan, pia anasema, ni namna ya kuhamasisha thamani ya kujitolea ambayo imesambaa katika nchi.

Baada ya siku tano za kutoa huduma kwa wakimbizi, vijana hao watakwenda katika Chuo Kikuu cha MADABA kilicho anzishwa kwa matashi ya Baba Mtakatifu Mtaafu Benedikto XVI. Kwa siku tatu watafanya jukwaa juu ya mada ya elimu ya amani na mazungumzo ya kidini hadi tarehe 25 Septemba 2017. Na katika  jukwaa lao wamealika wawakilishi wa serikali mahalia, Mfalme wa nchi hiyo na Balozi wa Kitume wa Papa nchini Jordan.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.