2017-09-19 13:27:00

Shukrani kwa Padre Majewski Mkurugenzi wa Vipindi vya Radio Vatican


Katika kujikitia kwenye shughuli za kila siku katika Jengo la Pio, limetufanya kukutana na sura ya Padre Adrzej Majeweski wa Shirika la Wayesuit. Kwa miaka hii ametusindikiza katika harakati za kupiga hatua za kwanza ya mageuzi, ambayo pia imegusa Radio Vatican. Ni kwa mujibu wa maneno ya Baba Mtakatifu Francisko kuwa “ lazima kufikiria kwa muundo na aina mpya inayostahili katika hali ya sasa ya teknolojia na mahitaji ya nyakati za sasa”. (Hotuba ya Papa Francisko, 4 Mei 2017).

Hayo ni maneno yaliyoandikwa kwenye barua ya Monsinyo Dario Vigano Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican na Katibu wake  Monsinyo Ruiz kwa ajili ya  kumuaga Padre Adrzej Majewski. Barua inaendelea kusema; Padre Andrej anawakilishwa Taasisi ya Radio Vatican  tangu mwaka 1984 hadi 1986, akiwa anafanya mazoezi ya vipindi vya Radio kwa lugha  ya Kipoland. Baadaye alichaguliwa kuwa mkurugenzi wa vipindi vya lugha ya kipoland kuanzia mwaka 1991-2001. Hatua ya tatu katika shughuli za  katika Radio Vatican ilianza mwaka 2015 ambapo aliteuliwa kuwa mkurugenzi msaidizi wa vipindi vyote vya  Radio Vatican, na tarehe 29 Septemba ya mwaka huo akawa Mkurugenzi wa vipindi vyote vya Radio Vatican.

Kwa njia hiyo mara baada ya uzoefu huo katika Radio Vatican, Padre Adrzej Majewesk anafikia hatua nyingine ya kuhama kwenda kuhudumia Kanisa kwa uaminifu kama alivyosema Mtakatifu Ignatius  wa Loyola mwanzilishi wa Shirika lake kuwa “Binadamu ameumbwa kwa ajili ya kusifu, kuomba na kutoa huduma kwa Bwana wetu Yesu Kristo ili kuweza kufikia ukombozi ”. Kwa njia hiyo Padre Andrzej anarudi Warsaw, Poland katika Chuo cha Wayesuit mahali alipoanzia akiwa kama Gombera kwa miaka mitano kabla ya kuja Roma.

Aidha Padre  Majeweski kabla ya kuja Roma amejikita kwa miaka mitano kama mkurugenzi wa vipindi Katoliki katika televisheni ya Taifa ya Poland (TVP). Pia alifanya kazi kama Mkurugenzi wa  Kituo cha Mawasiliano Ulaya na Utamaduni huko Warsaw, pia katika Kituo cha mafungo ya Kiroho cha Wayesuit  huko Poland. Hatua ya kuondoka katika mawasiliano ya Radio  Vatican, yanampeleka kwa mara nyingine kushirikiana na Radio ya Taifa huko Poland, wakati huo huo atajishughulisha na utume kichungaji na huduma nyingine ambazo ataombwa kufanya katika Chuo cha Wayesuit huko Poland. Monsinyo Vigano na Ruiz wanasema, hiyo ni kuonesha kwamba kila aliye tayari kuwajibika hakosi kamwe kazi ya kufanya.

Padre Adrzej Majewski ataacha shughuli ya Ukurugenzi wa Radio Vatican tarehe 29 Septemba 2017. Kwa njia hiyo Monsinyo Viganò na Monsinyo A.Ruiz wanachukua fursa hiyo kumshukuru kwa ushirikano wake, uaminifu wa kazi alio uonesha bila kuchoka. Pia hawakusahau shughuli nyeti aliyo wasindikiza wafanyakazi wa Radio Vatican kwa urafiki na upendo. Wanamtakia mafanikio mema na kutoa ahadi ya kumsindikiza kiroho katika kazi mpya ambayo amekabidhiwa.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.